JK Aagiza Shule za sekondari , Vituo vya Afya Kuunganishiwa Umeme.

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhahakisha kuwa shule zote za sekondari za kata, zahanati na vituo vyote vya afya nchini kuwekewa umeme haraka iwezekanavyo.

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhahakisha kuwa shule zote za sekondari za kata, zahanati na vituo vyote vya afya nchini kuwekewa umeme haraka iwezekanavyo.

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhahakisha kuwa shule zote za sekondari za kata, zahanati na vituo vyote vya afya nchini kuwekewa umeme haraka iwezekanavyo.
Rais Kikwete amesema kuwa kwa maeneo yenye umeme wa Gridi ya Taifa, taasisi hizo za umma zipatiwe umeme kutoka kwenye Gridi hiyo na kwa maeneo yasiyokuwa na umeme wa Gridi basi shule na taasisi hizo nyingine ziwekewe umeme wa nguvu za jua (solar).
Rais pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya kusimamia ipasavyo programu ya kusambaza umeme na maji katika vijiji mbali mbali nchini akisisitiza kuwa lengo la kuwapatia umeme Watanzania asilimia 30 ifikapo mwaka 2015 linaweza kufikiwa na kupitwa vizuri kama viongozi wanajipanga vizuri.
“Ni jambo la ajabu mama zetu wanakwenda kujifungua kwenye kituo cha afya na wanalazimishwa kubeba taa ama chemli ya kuongeza mwanga wakati wa tendo la kujifungua. Nchi hii haina umasikini wa kiasi hicho,” Rais Kikwete amewaambia viongozi wa Mkoa wa Pwani.
Akizungumza na viongozi wote wa Mkoa huo leo, Alhamisi, Oktoba 10, 2013 kwenye Hoteli ya Oceanic Bay mjini Bagamoyo katika majumuisho ya ziara yake ya siku sita kukagua na kuzindua shughuli za maendeleo, Rais Kikwete amesema:
“Moja ya mambo ambayo nataka nyie viongozi wa Mkoa huu na mikoa mingine ya nchi yetu wafanye haraka iwezekanavyo ni kuunganisha shule zetu zote za sekondari, zahanati na vituo vya afya kwenye mtandao wa umeme,”
Ameongeza: “Kwa zile shule zilizoko katika maeneo yenye umeme wa Gridi, nataka umeme huo uvutwe kutoka kwenye Gridi hiyo na kwa maeneo pasipokuwa na umeme wa Gridi tutumie umeme wa nguvu za jua. Kwa shule yenye vyumba vinane, gharama ya kuweka umeme ni Sh. milioni nne na kwa kituo cha afya ni Sh. 12,000,000. Hizi ni pesa tunaziweza kabisa.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Kwa hakika, hatuwezi sisi kama taifa kuendelea na shule zisizokuwa na umeme kabisa wakati tukijipanga vizuri, tunaweza kulimaliza hili haraka. Tuko karne ya 21.”
Kuhusu usambazaji wa umeme na maji katika vijiji mbali mbali vya Tanzania, Rais Kikwete amesema kuwa maadamu kazi hiyo sasa imepamba moto, wajibu mkubwa wa Wakuu wa Wilaya sasa ni kusimamia na kuhakikisha kuwa vijiji ambavyo vinatakiwa kupatiwa umeme na maji vinapata huduma hiyo haraka na kwa wakati bila kuchelewa.
“Mpango huu ni kusambaza umeme na maji katika vijiji vyetu ni mkubwa mno na ambao haujapata kutokea katika historia ya nchi yetu. Tulipoingia madarakani ni asilimia 10 ya Watanzania waliokuwa wanapata umeme. Sasa tumefikia asilimia 21 katika lengo letu la kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2015. Lakini naamini kuwa tunaweza hata kufikia asilimia 40.”
Rais Kikwete amerejea Dar es Salaam leo baada ya kumaliza ziara hiyo yenye mafanikio.