KUNDI la Ngoma Africa Band aka ‘FFU’ Ughaibuni, linatarajiwa kuendelea kumwaga burudani zake Ulaya na safari hii ni kwa mashabiki wa mjini Tuttlingen, show itakayofanyika Jumamosi ya Agosti 27, 2011
Bendi hiyo maarufu kwa muziki wa dansi barani Ulaya yenye maskani yake nchini Ujerumani, inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho lingine kubwa la Afrika Festival, mjini Tuttlingen, Ujerumani ya Kusini, Kamanda Ras Makunja kiongozi wa kikosi hicho amebainisha.
Bendi hiyo inayotajwa kama pekee ya kiafrika barani Ulaya inayoweza kuwapagaisha mashabiki wa kimataifa kwa wingi, pia kutumia muziki wake made in bongo uswahilini kama daraja au urimbo wa kuwanasana washabiki katika kila kona duniani, na kuwapa burudani ya aina yake.
Wakali hawa wa muziki wa dansi kwa sasa wanatamba na nyimbo zao mbili mpya “Bongo Tambarare” na “Supu ya mawe” wasikilize zaidi at www.ngoma-africa.com tafadhali usisahau ku-log in at www.ngoma-africa.com