Jifunze kutafuta simu yako kupitia Google

Namna ya kutafuta simu yako kupitia Google.

Inatokea mara nyingi umeweka simu yako mahali na baada ya muda kidogo unasahau kuwa umeiweka wapi. Ukiwa upo nyumbani sio hatari, ila kama umekaa bar, simu yako inaweza ikawa mikononi mwa watu wasiokutakia mema. Kwa kutumia google unaweza ukafanya mambo yafuatayo.

  • Ukapiga simu (simu yako itaita hata kama ipo kwenye vibration)
  • Uka ukaifunga (lock) simu yako
  • Ukafuta data zote zilizopo kwenye simu.
Nenda kwenye google na tafuta "where is my phone"

Nenda kwenye google na tafuta “where is my phone”

Ili iweze kufanya kazi, unatakiwa uwe umewasha location kwenye simu yako.
Kama umepoteza simu yako, au umeisahau nyumbani na unawasiwasi hujaifunga, unaweza kufanya yafuatayo.

  • Log in kwenye google.com kutumia account ambayo unatumia kwenye simu yako ya android.
  • Nenda kwenye google search na tafura “where is my phone”
Unaweza kupiga, kufunga au kufuta data kutoka kwenye simu yako

Unaweza kupiga, kufunga au kufuta data kutoka kwenye simu yako

Google itatafuta simu yako na itakupa option nilizozitaja hapo juu.

Kama umeipenda hii post, ni follow kwenye instagram @muzegroup, tips nyingine kama hizi zinakuja.