MFALME wa muziki wa reggae barani Afrika, Jhikoman amefanikiwa kufunika kwa kishindo katika maonesho ya 5th International African festival Tubingen, yaliyofanyika Jumapili ya Julai 20, 2014 mjini Tubingen, Ujerumani.
Katika onesho hilo mwanamuziki Jhikoman kwa sasa ndiye nyota inayong’aa kutoka Afrika kwenye muziki wa reggae na aliudhihirishia ulimwengu kuwa Tanzania ni moto wa kuotea mbali kimuziki, huku akishagiliwa na umati wa washabiki waliofika kwenye maonesho hayo.
Jhikoman anatajwa kuwa ndiye mfalme na nyota mpya wa muziki wa reggae kutoka Afrika, Jhikoman mwenye maskani yake Bagamoyo mkoani Pwani, Tanzania amepata bahati ya kukubalika na kupata mkataba wa kutumbuiza katika maonyesho mengi barani ulaya.