Jhikoman Atingisha International African Festival Ujerumani

Jhikoman alikaribishwa na wasomi wa muziki ambao wanamapenzi na Tanzania na watakuja Bagamoyo project maalumu

Tubingen,Ujerumani,

Mwanamuziki maarufu wa reggae barani Afrika Jhiko Manyika aka Jhikoma kutoka Bagamoyo,Tanzania,alifanikiwa kuwadatisha akili washabiki wa muziki nchini ujerumani siku ya alhamisi 17 julai 2014 katika maonyesho makubwa ya kimataifa 5th International African festival Tubingen 2014,yanayofanyika katika viwanja vya Festplatz,mjini Tubingen,Ujerumani.

jhikoman kazini

Mfalme wa Reggae Jhikoman akifanya vitu vyake
Mwanamuziki huyo nguli wa reggae amepewa heshima zote za kimataifa kwa uwakilishaji wake kama balozi wa reggae wa Afrika.ratiba ya maonyesho hayo inaonyesha kuwa Jhikoman atapanda tena jukwaani siku ya jumapili 20.Julai 2014 jioni kwa ajili ya maombi maarumu ya washabiki waliotaka kumuona tena mflame huyo wa reggae.
Pia taarifa zimetosha kuwa jumamosi 19 julai 2014 saa 2.00 usiku FFU-Ughaibuni aka Ngoma Africa band watatumbuiza katika maonyesho hayo.

Mfalme wa Reggae Jhikoman akifanya vitu vyake