SIKU chachea baada ya mfanyabiashara maarufu nchini na mwanachama wa Simba SC, Mohammed Dewji ‘Mo’ kuichangia klabu hiyo shilingi milioni 100 za usajili, hatimaye wamefanikiwa kumleta mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo.
Mavugo ambaye ametokea nchini Ufaransa alikokwama kujiunga na klabu ya Tours ya Ligi Daraja la Pili, maarufu kama Ligue 2 ametua usiku wa Jumatano August 3 jijini Dar es salaam kwa ajili ya kumalizana na Wekundu hao wa Msimbazi wenye agenda nzito ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.
Straika huyo ambaye amezungumzwa kwa muda mrefu kujiunga na Simba na kufikia hatua watani zao wa jadi kuanza kuwatania kwa jina la ‘Wazee wa Mavugo’ amepokelewa na makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu.
Inaonekana Mavugo atakuwa akivaa jezi namba 45 mara atakapokamilisha usajili wake, bahati nzuri uhakika upo kutokana na mkwanja aliomwaga MO.
Chanzo:shaffihdauda.co.tz