UMOJA wa Mataifa unasema kuwa Jeshi la Sudan Kusini limewapiga risasi na kuwauwa watu 10, ambao walikuwa wakiandamana kupinga kuhamishwa kwa Makao Makuu ya Serikali za mitaa magharibi mwa nchi.
Ofisa wa kuweka amani wa Umoja wa Mataifa huko Bahr el-Ghazal amesema watu wane waliuwawa katika mji wa Wau kwenye mapambano ya jana usiku. Na wengine sita waliuwawa baada ya kukusanyika kulalamika juu ya mauaji ya awali. Hata hivyo Jeshi la Sudan Kusini limekataa kusema chochote.
Wakati huo huo; wawakilishi wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wameanza mazungumzo na wapiganaji wa M23 mjini Kampala, Uganda. Viongozi wa Maziwa Makuu wakikutana Kampala mwezi Februari pamoja na Rais Kabila (kushoto)
Waziri wa Ulinzi wa Uganda, Crispus Kiyonga, alisema huo ni mwanzo wa majadiliano baina ya pande hizo mbili. Wapiganaji wa M23 waliondoka mjini Goma, mashariki mwa Congo, siku nane zilizopita, lakini walitishia kurudi iwapo madai yao hayatasikilizwa.
Rais wa Congo, Joseph Kabila, ameahidi kusikiliza malalamiko yao. Malaki ya watu wamehama makwao katika ghasia tangu wapiganaji hao walipoasi na kutoka katika jeshi la Congo mwezi wa Aprili.
-BBC