Utata huo uliojitokeza katika taaarifa ya tukio hilo la ujambazi iliyotolewa na Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa,Akili Mpwapwa jan alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Mpwapwa alisema kuwa watu hao ambao wanaodhaniwa kuwa ni majmbazi waliuwawa
na wananchi wenye hasira kali kwa mawe katika eneo la Matejoo mara baada ya kulitekeleza gari walilokuwa wakilitumia na kisha kukimbia kwa miguu.
Mpwawpa alidai kuwa hadi sasa jeshi hilo halijaweza kuwatambua kwa majina majambazi hao,hukua akibainisha kuwa marehemu hao wametambulika kuwa ni wahalifu na wamehusika katika vitendo mbalimbali vya uhalifu jijini hapa huku mmoja kati yao akihusishwa katika tukio la uporaji lililotokea eneo ya maji ya chai.
Hatahivyo,mara baada ya maelezo ya Kaimu huyo,baadhi ya waandishi wa habari walitaka kujua undani wa taarifa juu ya majambazi hao,na kufika katika chumba cha
kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa ya Mt,Meru ambapo walipatiwa majina ya marehemu hao na wahudumu wa chumba hicho.
Wahusika wa chumba hicho waliwataja marehemu hao kuwa ni Obeid Erasto(30),Raphael Patrick(37) na
majambazi hao wakiwa na gari lenye namba za usajili T785 ACM aina ya Toyota mark II waliwateka wafanyabiashara hao watano waliokuwa kwenye gari aina ya Hyundai lililokuwa na namba
Alkili alidai kuwa baada ya kufanikiwa kupora walirusha risasi mbili hewani na kugeuza gari lao kurudi mjini Arusha lakini wakati wakirudi wananchi waliokuwa karibu na eneo la tukio walitoa taarifa kwa jeshi la polisi na kisha jeshi hilo kufanya jitihada za kuzuia njia zote za kuingilia katikati ya mji wa Arusha.
Alisema kuwa majambazi hao walipofika katika eneo la Matejoo mjini Arusha walipoona wanafuatiliwa ndipo waliamua kulitekeleza gari walilokuwa wakilitumia na kisha kuanza kukimbia kwa miguu hali iliyopelekea wananchi kuwafukuza na kufanikiwa kuwakamata ambapo waliwapiga kwa mawe na kudai kuwa walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitalini na polisi
Kaimu huyo alisema mmoja kati yao alikutwa na bastola aina ya Browning yenye namba 069082 ikiwa na risasi 3 huku 4 zikiwa zimeshatumika.
Alisema kuwa upekuzi uliofanywa na jeshi hilo ndani ya gari walilokuwa wakitumia majambazi hao walikuta silaha aina ya pump action Mossberg yenye namba R273578 ikiwa na risasi 14 na silaha ya kienyeji aina ya Rifle 458 ikiwa na risasi 3.
Aliwataja wafanyabiashara waliotekwa na kuporwa fedha hizo kuwa ni Silas Soyolo maarufu kama “Mollel”(40),Gregory Joseph(39),Jackson Kisioki(47),Lembris Bikoto(60) pamoja na Jackson Kalaine(35) wote wakazi wa Arusha.
mpwapwa alisema uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kubaini mmilikiwa gari walilokuwa wakitumia majambazi hao.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Arusha Akili Mpwapwa akionyesha silaha walizokutwa nazo majambazi watatu waliouwawa na wananchi baada ya kupora zaidi ya shilingi milioni nne kwa wafanyabiashara,kushoto ni Rifle 458 iliyokuwa na risasi 3 na kulia ni Pump Action Mossberg iliyokuwa na risasi 14)
Picha na Janet Mushi