Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Mh. Jerry Silaa akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chimbo
School of Thought ambaye pia ni mtangazaji wa redio Clouds na TV
Harris Kapiga wakati alipofika kwenye chimbo hilo kuzungumza na vijana
baada ya kuitikia mwaliko kutoka kwa Mwenyekiti
huyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Mh. Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa
Mwenyekiti wa Chimbo School of Thought ambaye pia ni mtangazaji wa
redio Clouds na TV Harris Kapiga.
Mmoja wa vijana akimuuliza maswali Mstahiki Meya
Jerry Silaa.
Na Mwandishi Wetu
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Mh. Jerry Silaa akiwa katika ya nchi ya Ahadi Sinza Kamanyola
amefunguka kuhusiana na namna gani kijana anaweza kuishi ndoto
zake.
Moja ya mambo aliyoyazungumzia ni pamoja na kijana
kujitambua na kujua nini hasa anataka na anapata vipi kwa maandalizi
ya kutimiza nia yake.
Mh. Jerry pia amechambua mada hiyo kwa marefu na
vijana kuonekana kumuelewa ipasavyo na hivyo kubaki kazi kwao
kutekeleza na kuyafanyia kazi yale aliyoyazungumza, ikiwemo kujua
lengo lao hasa ni nini na kujipima wanautayari wa kiasi gani katika
kutekeleza hilo lengo na kubwa zaidi ni uthubutu wa kufanya jambo
lenyewe.
Katika mazungumzo yake kilichowavutia vijana wengi
zaidi ni pale alipowaeleza kuwa yeye Mstahiki alithubutu kugombea
udiwani ndani ya kata ya Ukonga akiwa na umri wa miaka 23 na
kufanikiwa kushinda.
Ni jambo la kujivujia kuwa na vijana hasa kama
mstahiki Jerry Silaa ambaye pamoja na kuwa Mstahiki Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu na
Kamati Kuu ya Chama tawala cha CCM Taifa.
Pamoja na hayo Mh. Jerry Silaa amewaeleza vijana
kutambua hizo ndoto ni za nani hasa na ni nani wakuzifanikisha kama si
wenyewe.
Aidha, zaidi ya hapo amewaasa vijana kuwa na majibu
ama matokeo ya kila wanalofanyia kazi “being result oriented” na
kupata kile wanachokitaka kwa kuzingatia lengo pamoja na muda
kiutendaji.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Mh. Jerry Silaa katika picha ya pamoja na vijana waliojitokeza
kumsikiliza wakati akifunguka kuhusuiana na namna gani kijana anaweza
kuishi ndoto yake.