Jenerali Mtaafu Hashimu Mtezo Afariki Dunia

Brigedia Jenerali (mstaafu) Hashimu Said Mtezo

Brigedia Jenerali (mstaafu) Hashimu Said Mtezo


JESHI la Ulinzila Wananchiwa Tanzania (TWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali (mstaafu) Hashimu Said Mtezo kilichotokea tarehe 04 Oct 14 kwa ugonjwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Dar es Salaam alipokuwa akipata matibabu.

Alizaliwa Machi 18, 1945 Wilayaya Dodoma mjini katika Mkoa wa Dodoma, alisoma katika shule ya Sekondari ya Tabora kuanzia mwaka 1962 hadialipohitimu Kidato cha Sita mwaka 1967. Alijiunga na Jeshi la Wananchiwa Tanzania tarehe 20 Juni, 1968. AlitunukiwaKamisheniJuni 05, 1969.

Katika utumishi wake Jeshini, alihudhuria na kufaulu kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi. Marehemu Brigedia Jenerali Mtezo amewahi kushika madaraka mbalimbali, Mwambata Jeshi nchini Zimbabwe 1987 hadi 1993, Mkurungenzi wa Mafunzo Makao Makuu ya JWTZ 1993 hadi 2002. Hadi anafariki alikuwa amestaafu Juni 30, 2002 baada ya kulitumikia Jeshi kwa muda wa miaka 34. Mazishi yanafanyika leo tarehe 07 Octoba, 2014 Mbezi Lous.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
BRIGEDIA JENERALI HASHIMU SAIDI MTEZO (MSTAAFU)
AMINA.
ImetolewanaKurugenziyaHabarinaMahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
Dar es Salaam, Tanzania.