Leo ni siku ya Baba hapa Marekani, na TheHabari inapenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza mababa wote duniani. Hii ni siku ambayo ina enzi malezi ya baba na ushawishi wake katika jamii. Siku ya Baba, ni siku ambayo inasheherekewa na nchi mbalimbali katika jumapili ya tatu ya mwezi wa Sita, na nchi nyingine huwa inasheherekewa miezi mingine tofauti.
Katika pekua pekua, TheHabari ilikutana na Jarida kwenye mtandao wa “Match.com” linalo elezea alama sita kwa wanawake kujua kama mwanaume fulani anazo chembechembe za kuwa ‘baba mzuri’ wa watoto wake hapo baadae. Jarida hilo linazitaja dalili hizo kama ifuatavyo:
1) Mwanaume huyo ana mahusiano mazuri na mama yake. Katika kipengele hiki, wakati mwanamke anatafuta baba mzuri wa watoto wake anabudi kujiuliza maswali yafuatayo zidi ya mwanaume husika…. Je ana mheshimu mama yake? Je ana cheka na mama yake kwa urahisi? Je anapenda kumtembelea mama yake? Je anamsaidia mama yake kazi ndogondogo za nyumbani? Kama majibu ya maswali haya yote ni “NDIYO!” Basi huyo mwanaume anazo chembechembe za kuwa baba mzuri wa watoto hapo baadae.
2) Mwanaume huyo sio mbinafsi. Kitu cha kwanza mtu anajifunza anapokuwa mzazi ni kwamba hauna kipaumbele tena, kipaumbele kinakwenda kwa mtoto. Hivyo basi, katika kipengele hiki, mwanamke anatakiwa awe makini sana na mwanaume ambaye anataka yeye ndio afikiriwe na kuthaminiwa wakati wote. Jarida la ‘Match.com’ linaonya wanawake kukaa mbali na wanaume wa aina hii, kwani hawana sifa za kuwa baba wazuri hapo baadae.
3) Mwanaume huyo asiwe mtu wa kupata kichefuchefu kirahisi. Kipengele hiki kwa ufupi kinazungumzia wale ‘mabraza men’, ambao wakiona kinyesi cha mtoto wanakunja sura! Kama baba, kuna wakati unatakiwa umsaidie mama kubadilisha nepi, kwahiyo suala la kinyaa linawekwa pembeni hapa.
4) Ni mjomba mzuri. hiki pipengele kinasema kwamba kama mwanaume ni mtu mnyenyekevu kwa watoto wa dada zake na kaka zake, basi anazo chembechembe zote za kuwa baba mzuri wa watoto wake mwenyewe hapo baadae.
5) Haoni hatari kupokea maelezo kutoka kwa mwenza wake. kipengele hiki kinasema kama mwanaume ni mbishi wa kuambiwa lolote, basi itakuwa ni ngumu sana hapo baadae kupokea maelezo yoyote yanayohusiana na ratiba za watoto, mathalani shule na kadhalika.
6) Haoni hatari kucheza kidali Po!. Dalili hii ya mwisho inaonyesha kwamba mwanaume huyu achukulii maisha ‘serious’ sana, kiasi kwamba anashidwa hata kucheza na watoto, pale wanapomuhitaji. Kama unavjojua tena, watoto wana hulka ya utundu, na endapo kwa bahati mbaya wamemmwagia baba mchuzi kwenye shati lake wakati anajiandaa kwenda kazini. Baba anatakiwa awe ni mtu mwepesi wa kuelewa na pia mcheshi.
dalili ndiyo hizo wadau, na bila shaka zina chembechembe za ukweli ndani yake, kwahiyo kazi kwenu!
Habari hii iliandikwa kwa kingereza na Muandishi Erika Rasmusson Jane wa New York na kutafsiriwa kwa Kiswahili na TheHabari.