Je, Wanawake ni Mabingwa wa Kuzuga Kitandani?

wapenzi wakiwa faragha

wapenzi wakiwa faragha

 

KAMA wewe ni mwanaume, basi bila shaka unafahamu ile milio na miguno ya wanawake wakati wa kujamiiana, na kama wewe ni mwanamke pia unafahamu kwamba huwa unatoa milio na miguno hiyo. Ni nini basi kinachopelekea milio na miguno hii kutolewa? Je milio na miguno hii ni ya kweli au ni zuga tu, ili kumfanya mwanaume ajisikie “kijogoo“?

Baadhi ya wataalamu wa masuala ya kujamiiana na mapenzi walijiuliza pia maswali hayo. Mwaka jana, Gayle Brewer wa Chuo Kikuu cha Central Lancashire na Colin Hendrie, wa Chuo Kikuu cha Leeds waliibuka na utafiti wao waliouita “Copulatory Vocalization“ (kwa tafsiri nyepesi-“Milio/sauti za kujamiiana”). Katika utafiti huo, waliuliza wanawake 71 ambao wanashiriki tendo hilo mara kwa mara (sexually active) kati ya umri wa miaka 18 na 48 kwa ajili ya kupata undani zaidi wa suala hili la kutoa milio wakati wa kujamiiana.

Wataalamu hao waliweza kubaini kwamba wengi wa wanawake hao walikuwa wanatoa milio, lakini sio tu wakati wanafika kileleni (orgasm), bali 66% walisema walitoa milio, ili kuharakisha wanaume zao kufika kileleni, na 87% walisema kwamba walitoa milio, ili kumfanya wanaume ajisikie “Kijogoo” (boost his self-esteem).

Wataalamu hao waliongeza kusema kwamba “Wakati mwanamke kwa kawaida hufika kileleni wakati wa kutomasana, mara nyingi milio ya kujamiiana imeripotiwa kutokea mara kwa mara kabla au sambamba na wakati ambao mwanaume anafika kileleni“. Walisema pia katika utafiti wao imebainika kwamba wakati mwingine wanawake walitoa milio na miguno, ili kukabiliana na kuboheka, uchovu, na maumivu wakati wa tendo la ndo, kwahiyo basi wanaume inabidi kuwa makini kwani wakati mwengine kumbe mtoto wa watu ana umia! Au pengine yupo kwenye zile harakati za kukuzuga, ili ujione “Kijogoo”?

Wataalamu wanaendelea kusema kwamba tatizo kubwa ni kwamba jamii imefanywa kuamini kwamba milio wakati wa tendo la kujamiiana huusishwa na mwanamke kufika kileleni  au kufurahia tendo hilo, kiasi kwamba imefikia wanawake kuona ni busara kudanganya (fake) kwamba wamefika kileleni (wakijua fika kwamba mwanaume tayari ana amini hivyo) wakati kumbe hawajafika popote.

Wataalamu wanaonya kwamba sio busara kwa wanawake kudanganya kwamba wamefika kileleni, kwani kufanya hivyo kunapelekea wanaume kufikiri kwamba wanafanya kila kitu sawa wakati wa mapigo, wakati kumbe sio. Mwalimu wa elimu ya kujamiiana, Patty Brisben, anashauri kwamba wanawake watumie miguno/milio kama “njia ya kuonyesha kwamba wanafurahia tendo, lakini sio njia ya kuficha kama tendo hawalifurahii.”

Kuficha au kutokuficha, wataalamu wanasema kwamba suala la kutoa milio/miguno wakati wa tendo la kujamiiana sio suala la binaadamu peke yao, utafiti kwa wanyama umebaini kwamba hata manyani jike (baboons) hutoa milio fulani kabla au wakati wa tendo hilo. Nyani jike hutoa milio fulani kuhashiria kwa nyani dume kwamba yupo tayari kwa tendo hilo na pia manyani jike huongeza milio wakati wanajamiiana na nyani dume, ambae ana cheo katika kundi lao (higher-ranked male baboon). Zaidi ya hayo, nyani jike aina ya “Macaque” amebainika pia kutoa milio/miguno wakati wa tendo hili nyeti, ili kumfikisha mwenza wake kileleni haraka!

Mwisho wa yote wataalamu wanamalizia kusema kwamba suala la kuridhishana kimapenzi (tuite “ukijogoo” wa mwanaume au vinginevyo), ni suala muhimu kwa pande zote mbili, yaaani mwanaume na mwanamke. Kwahiyo basi, suala la kutoa milio sio tu suala la mwanamke kudanganya au kufanya mambo asiyotaka, bali ni suala la kuwepo “hai” (sexually present) (mara ngani umeshasikia wanaume wa kitanzania wakilalamika kuhusu wanawake wanaokaa kama “gogo” au “kusoma gazeti” wakati wa kujamiiana??) wakati wa tendo hilo na kubadilishana mahaba na mwenza wake.

Mwisho kabisa, wanasema, “wote (wanaume na wanawake) tutoe milio!”

Je unakubaliana na utafiti huu?

Source: CNN Health

Muandaaji: www.thehabari.com