JE ALIYELALA AAMSHWE?

Huyu si mwingine bali ni waziri mwenye dhamana ya kuiongoza wizara ya nishati madini mheshimiwa sana bwana William Ngeleje, waziri ambaye wizara yake imekuwa ikilalamikiwa kwa ufisadi na utata katika mikataba feki , pembeni kabisa mwa bosi wake na mkuu wa nchi, tena kwenye mkutano wa kimataifa, jionee mwenyewe jinsi anavyouchapa usingizi bila hata kuwa na shaka na wasi, kwa mwendo huu wa usingizi kweli ataweza kuipitia mikataba ya madini na nishati kwa uangalifu! kazi ipo hapa, shibe ikizidi haya ndiyo matokeo yake. Kwa sisi tuliozoea kula mlo mmoja kwa siku, ni nadra sana kupata usingizi kirahisi hivi, lakini pengine ni uchovu wa safari tusimlaumu sana waziri wetu mpendwa.