BINGWA wa mchezo wa Kick Boxing nchini, Japhert Kaseba ameingia katika fani ya filamu za mapigano ‘live’ akianzia na picha yake ya kwanza itakayo mtambulisha inayotambulika kwa jina la “Bongo Mafia”
Filamu hiyo iliyo rekodiwa katika ubora wa hali ya juu sasa ipo mtaani ikisambazwa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya wapenzi wa filamu nchini wajionee vitu tofauti vilivyoandaliwa na wakali kibao walioshirikishwa.
Akizungumzia filamu hiyo Kaseba alisema picha hiyo ni mfululizo wa picha nyingine kibao ambazo zipo njiani, kwani amebainisha kuwa amekuja kufanya kazi katika jamii ili watazamaji wenyewe waweze kutoa maoni yao.
Alisema ‘Bongo Mafia’ imewashirikisha wasanii kama Dotnata, Kelvin, Muhogo Mchungu, Pendo Njau Champion na Rogers MASTER SHIVO, na Wasanii wengine kibao. Amesema filamu hiyo kwa sasa ni gumzoo mtaani wakati ndio kwanza inamaliza wiki moja tangu kuingia sokoni.
Kaseba ambaye hivi karibuni ali mdunda bondia Rasco Simwanza wa Malawi amejitamba kuendeleza ubabe kwa mabondia wengine huku akifanya kazi zake za sanaa ambazo kwa kiasi kikubwa anamshukuru sana Dotnata kwa kuona kipaji chake hicho ambacho kilikuwa kimejificha na sasa kipo mtaani.
Kaseba amesisitiza kwa mashabiki wake wamuunge mkono kwa kununua kazi hiyo kwani ndio kwanza ananza kulishika soko la filamu hapa nchini endapo watajitokeza na kumuunga mkono, ndipo watakapofuraia kazi zake nyingi zilizopo jikoni. “Nina kazi tofauti tofauti nne hivi na sijui nianze na ipi ndio maana nimeamua kutoa hii kwanza,” alisema Kaseba