Na Mwandishi Wetu, Arusha
MASHIRIKA mawili yasiyokuwa ya kiserikali (NGO’s) yanayotoa msaada na ushauri wa kisheria kwa jamii za kifugaji na wawindaji na kutetea haki zao, yametoa msaada wa zaidi ya sh. milioni 7 kwa ajili ya ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Yaedachini wilayani Mbulu.
Mashirika hayo ni PINGO’s Forum na UCRT ya mkoani Arusha, ambapo
wametoa mabati 100 na mifuko 100 ya sementi kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya wanafunzi wa kike na kiume ambao hivi sasa baadhi yao wanaishi nje ya shule kutokana shule hiyo kutokuwa na mabweni.
Mkurugenzi wa Miradi wa Pingo’s, Isaya Naini na Mwanasheria
wa UCRT, Edward Lekaita wakizungumza katiak hafla ya makabidhiano hayo yaliyofanyika shuleni hapo, walieleza kuwa wameguswa kuisadia sekta ya ya elimu kutokana na kuguswa na mazingira hatarishi wanayoishi wanfunzi hao. Aidha kampuni inayojihusiha na huduma za kitalii ya Ndorobo Tours imechangia mifuko 50 ya sementi kwa ajili ya ujenzi wa mabweni hayo.
Aidha wadau hao wa maendeleo Yaedachini walisisitiza viongozi wa
serikali kutambua uhuhimu wa wa kuwasaidia kwa kuwapatia elimu watoto wa jamii ya kifugaji na ya wawindaji ambao wameachwa nyuma katika sekta hiyo muhimu ya elimu kutokana mazingira wanayoishi.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Mbulu Anatory Choya akizungumza baada ya kukabidhiwa misaada hiyo alisema atasimamia utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi wa mabweni ili kuboresha mazingira ya kusomea na ubora wa taaluma kwa wanafunzi hao.
Mkuu huyo aliwataka watumishi wa umma kuwa tayari kufanya kazi katika kituo chochote anachopangiwa na kuwaonya wenye tabia ya kukataa kwenda au kutoroka muda mfupi baada ya kuripoti kwa
madai ya mazingira magumu, huku tayari wamechukua posho za kujikimu na usafiri kuacha mara moja kwani serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa elimu sekondari wilayani
Mbulu, Michael Hadu, alisema walimu wawili waliopangiwa kufundisha
katika shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 141 walitoroka kituo chao
cha kazi siku baada ya kuripoti huku tayari wakiwa wamepokea posho ya kujikimu, usafiri na mizigo.