JAMBO LEO MABINGWA NSSF CUP

Timu ya mpira wa miguu ya Jambo Leo ikisherehekea kombe la NSSF Cup baada ya kulitwaa juzi.

TIMU ya soka ya Jambo Leo ‘Wagumu Star’ inayomilikiwa na kampuni ya Jambo Concepts Ltd, imetwaa Ubingwa wa Kombe la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya kuifunga timu ya NSSF katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Sigara Chang’ombe Dar es Salaam.

Katika mchezo huo mkali uliofanyika jana, timu ya NSSF ndio walio kuwa wa kwanza kupata bao dakika chache baada ya mchezo kuanza lakini muda mfupi baadae Jambo Leo ilisawazisha bao hilo kupitia kwa mchezaji wake Said Abdul na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilitoka uwanjani zikiwa na bao moja (1-1).

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikitafuta bao la kuongoza, lakini timu ya Jambo Leo ndio waliokuwa wa kwanza kuziona nyavu za NSSF kwani dakika ya 47 mchezaji wa Jambo Leo Stivin Waigaga aliipatia timu yake bao la kuongoza.

Mchezo uliendelea kuwa mkali kwani NSSF walikuwa wakitafuta bao la kusawazisha vhuku Jambo Leo wakitafuta lingine ili kuweza kujihakikishia ushindi, likini hadi mwisho wa mchezo timu ya Jambo Leo iliibuka na mabao mawili na NSSF moja.

Kwa ushindi huo timu ya Jambo Leo imejinyakulia kikombe cha mashindano hayo pamoja na fedha taslimu sh. 3,500,000. NSSF kama washindi wa pili wamejinyakulia sh. 2,000,000, huku washindi wa tatu timu ya Uhuru ikijipatia sh. 1,000,000.
Upande wa mpira wa pete kwa mashindano hayo timu ya Habari Zanzibar ndio imeibuka washindi na kupewa kikombe pamoja na fedha. jipatiameifunga Uhuru 1-0 matokeo ambayo timu ya Uhuru imeonekana kushukuru kwa kufungwa bao moja tofauti na walivyotegemea.

Timu ya Jambo Leo ambayo imekuwa ikigawa dozi ya mabao matatu mpaka saba kwa kila timu ambayo inakutana nayo, katika mashindano hayo kiasi cha kuogopwa; Jambo Leo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa mashindano hayo hadi imeingia fainali.

“Tunashukuru mungu sisi tumefungwa goli moja wenzetu wamekuwa wakifungwa 3, 4, hadi 7, hivyo tumejitahidi kwa matokeo haya…tumewabana kweli kweli,” alisema mmoja wa wachezaji wa timu ya Uhuru alipozungumza na HM. Mashindano hayo yanaendeleoa tena leo.