LEO nataka kuzungumzia masuala muhimu juu ya #DIETs ama namna ‘diets’ zinavyochukuliwa mwingine ukimuuliza kwamba diet ni nini atakujibu kushinda na njaa ama kujinyima chakula la hashaa!!
Maana halisi ni kula vyakula muhimu ama vinavyohitajika mwilini kwa mpangilio maaalum especially kwa watu wanaotaka kupunguza uzito, wanao umwa magonjwa mbali mbali pamoja na wanawake waja wazito na wanao nyonyonyesha.
Najua kwenye wajawazito mtakua mmeshtuka kwa kuwa tumeambiwa tangu na tangu ya kuwa tutaiathiri afya ya mtoto tukifanya diets pindi ni wajawazito si kweli kwa kuwa endapo ni mnene kupitiliza na unakula ovyo ya maanisha pia ni rahisi kuzaa mtoto asiye na afya na kuhatarisha afya yako kama mama na mtoto pia kwa kuwa na uzito mkubwa pamoja na mtoto na ndo maana kuna hadi mazoezi laini ya wajawazito ili wawe na afya njema yeye na mtoto (mazoezi aina ya yogani mazoezi mazuri mno kwa wajawazito)
.
Hivyo basi ninakushauri umuone Nutritionist akupangie vyakula sahihi na umuone angalau kila baada ya mwezi mmoja ili akushauri ni vyakula gani muhimu na sahihi kwa ajiri yako na mtoto aliye tumboni sababu wakati mwingi huwa ninaona akina mama wanakula vitu ovyo ovyo kusingizia ujauzito.
Wakati vitu vingi wanavyokula ni havihitajiki kwenye process nzima ya ujauzito na kumfikia mtoto ama havimsaidii mtoto aliye tumboni kwa namna yoyote kwa kuwa havina vitamins, minerals na virutubisho vyovyote vya kusaidia ukuwaji bora wa mtoto aliye tumboni.
Mfano mdogo tu kama soda, keki chips vitu vya kusindikwa ambavyo vingi watu huweka fleva tu na si vitu halisi n.k kwa ushauri zaidi waweza tuwatssap #0753320009
@kibongemwepec
Cc @witnesz_kibongemwepec