Jaji Warioba Ainadi CCM Butiama, Asema Imefanya Mengi…!

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Nyamuswa ambako ndiko alikozaliwa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli.

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Nyamuswa ambako ndiko alikozaliwa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli.

 Waziri Mkuu Mstafu Jaji Joseph Sinde Warioba akihutubia wakazi wa Butiama ambapo aliwaeleza Magufuli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
WAZIRI Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, ameibuka katika  kampeni za mgombea urais wa CCM Dk. John Magufuli na kusema kuwa anashangazwa na hatua ya mawaziri wakuu wenzake kuhama CCM na kudai hakuna kilichofanyika katika miaka 54 ya Uhuru.
Pamoja na hali hiyo amesema anajua wazi huenda hata wanachokifanya hawajui wajibu wao walipokuwa katika madaraka hayo kama washauri wakuu wa rais alisema  sasa umefika wakati wa watu wanaomtumia kama dira Baba wa Taifa katika kampeni zao wajitafakari zaidi.
“Wengine katika kampeni zao wanatumia maneno ya Mwalimu kama wamechanganyikiwa. Huwezi kumtumia Mwalimu kama dira halafu unasema CCM haijafanya kitu, aliijenga Tanzania kwenye misingi na wote walimfuata wanapita kwenye misingi yake,” alisema Jaji Warioba
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama
cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi
waliojitokeza katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika mjini Bunda.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipokea kifimbo na Chief Japhet Wanzagi kwa niaba ya Wazee wa Butiama.
 Dk. akionesha fimbo hiyo aliyokabidhiwa na Chief wa Wazanaki, Japhet Wanzagi
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge kulia ni Nimrod Mkono kutoka jimbo la Butiama Vijijini na  Profesa Sospeter Muhongo ambaye anatoka jimbo la Musoma vijijini.
 Mamia ya Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe
Magufuli.
 Mgombea Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mgombea Ubunge wa jimbo la Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe. Stephen Wasira,shoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba,kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika mjini Nyamuswa jioni ya leo.
 Wananchi wa Nyamuswa wakimsikiliza Dkt Magufuli.
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Nyamuswa ambako ndiko alikozaliwa
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba,wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgombea ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Ndugu Sospeter Muhongo,kushoto ni Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe. Stephen Wasira wakati wa mapokezi mkoani Mara,pichani kati ni Mtoto wa Baba wa Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki,Mh Makongoro Nyerere
  Umati wa wakazi wa Butiama wakimsikiliza Mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Sehemu ya Wananchi wa Butiama wakishangilia jambo. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MARA