Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman liyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland. Jaji Mkuu yuko Marekani kwa ziara ya kikazi
ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Kushoto ni mke wa
Rais Mama Salma Kikwete. Jaji Mkuu yuko Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo ili kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake waliopomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika
hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Jaji Mkuu na ujumbe wake wako Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya
Rufani, Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu, Ignass Kitusi, daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussein Katanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake (hawapo pichani) waliopomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Jaji Mkuu na ujumbe wake wako Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu, Ignass Kitusi, daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussein Katanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake (hawapo pichani) waliopomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Jaji Mkuu na ujumbe wake wako Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu, Ignass Kitusi, daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussein Katanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Meja Jenerali Adolph Mutta ambaye alimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman kwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ignass Kitusi ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Ibrahim Juma ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Jaji Mkuu na ujumbe wake wako Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. PICHA ZOTE NA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete Novemba 16, 2014 alikutana na kufanya mazungumzo na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman na ujumbe wake. Aidha, Rais Kikwete amewashukuru Watanzania kwa maelfu ya salamu za upendo kwake zikimtakia heri aweze kupona ambazo Rais amekuwa anapokea.
Rais Kikwete pia huenda akatolewa nyuzi katika siku tatu zijazo ikiwa maendeleo yake yataendelea kuwa ya kasi kama ambavyo imekuwa tokea alipofanyiwa upasuaji wa tezi dume Novemba 8, mwaka huu, katika Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore, Maryland, Marekani.
Rais Kikwete alikutana na kuzungumza na Jaji Othman na ujumbe wake waliofika kumjulia hali katika Hoteli Maalumu ambako Rais Kikwete anaishi baada ya kutolewa Hospitali. Hoteli hiyo iliyoko Baltimore ina uhusiano wa karibu na Hospitali ya Johns Hopkins.
Rais alimhakikishia Jaji Mkuu na ujumbe wake pamoja na Watanzania wote kwa ujumla kwamba hali yake imeimarika na kwamba anachosubiri sasa ni kuondolewa nyuzi katika sehemu aliyofanyiwa upasuaji.
Alisema kuwa baada ya kuondolewa nyuzi ndipo madaktari wake watakapofanya tathmini ya mwisho kabla ya kumruhusu kurejea nyumbani. Jaji Mkuu amekuwa kiongozi wa kwanza wa kitaifa kumtembelea Rais Kikwete toka alipofanyiwa upasuaji Novemba 8, 2014.
Rais Kikwete alimwambia Jaji Mkuu kuwa sasa afya yake imeimarika zaidi, huku akiendelea kufanya mazoezi kiasi cha mara nne ama tano kwa siku.
Rais amewakumbusha Watanzania kuhusu umuhimu kwa watu kuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili kuondoa shaka ya kupata tatizo kubwa kwa kuchelewa kugundua ugonjwa kwa wakati.
Alisema kwa upande wake yeye aliwahi kwenda kuchunguzwa na kwamba tatizo liligundulika mapema.
Kuhusu hali yake Rais amesema kwamba masharti ya daktari ni kwamba nyuzi za upasuaji wa tezi dume aliofanyiwa huondolewa siku 12 baada ya kufanyiwa huo upasuaji, na kwamba Novemba 20, 2014 ndiyo siku ambayo amepangiwa kurudi hospitali kufanya hivyo.
“Baada ya kuondolewa nyuzi madaktari watanifanyia tathmini ya mwisho na endapo kama kutakuwa hakuna tatizo lolote nitaruhusiwa kurudi nyumbani”, alisema Dk. Kikwete.
Jaji Mkuu na ujumbe wake wa watu wanne wako nchini Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo watahudhuria mkutano wa kimataifa wa kujadili mabadiliko ya sheria ya ushahidi pamoja na kukutana na taasisi mbalimbali za fedha, ikiwa ni juhudi za mahakama hiyo kupata wabia wa uendelezaji wa ujenzi wa taasisi hiyo.