Jackson Makwetta Afariki Dunia

Jackson Makwetta

MWANASIASA maarufu na aliyewahi kuwa Waziri katika wizara mbalimbali serikalini zikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi, Elimu, Kilimo na Utumishi, Bw. Jackson Makwetta amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa vyombo vya habari ni kwamba, Bw. Makweta amefariki dunia jioni ya Novemba 17, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ya jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa kwa matibabu.

“Serikali inasikitika kutangaza kifo cha Bw. Jackson Makwetta kilichotokea leo saa 11 jioni katika Msiba uko nyumbani kwake Boko kwa Wagogo. Taarifa zaidi kuhusu mipango ya mazishi zitatolewa baadaye. Bw. Makweta aliwahi kuwa Waziri katika wizara mbalimbali zikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu kama Waziri wa Nchi, Elimu, Kilimo na Utumishi. Pia amekuwa Mbunge kwa zaidi ya miaka 35,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.