Jack Wilshere Hang’oleki Atafia Arsenal

Jack Wilshere

Meneja Arsene Wenger amesema matumaini yake ni kwamba kiungo wa kati Jack Wilshere, ambaye kwa sasa ametumwa Bournemouth kwa mkopo, atasalia Arsenal maisha yake ya uchezaji.

Wilshere, 24, ambaye huchezea timu ya taifa ya Uingereza, alienda Bournemouth kwa mkopo wa msimu mmoja. Ni mmoja wa wachezaji waliokua kutoka chuo cha kustawisha wachezaji cha Arsenal na aliwachezea mechi yake ya kwanza 2008 akiwa na miaka 16.

Lakini alicheza mechi tatu pekee klabu hiyo msimu uliopita kutokana na majeraha.

Wenger amesema walizungumza na mchezaji huyo huku akitarajia kushuka dimbani watakapokutana na West Bromwich Albion kesho Jumamosi