Ivory Coast yakaribia kufanya uchaguzi

Wananchi wakiandamana nchini Ivory Coast wakati wa machafuko

JUMUIA ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, inasema kuwa itatuma ujumbe wa wachunguzi 60 kusimamia uchaguzi wa bunge nchini Ivory Coast Desemba 11, 2011 kufuatia ombi la serikali ya nchi hiyo.

Huo ni uchaguzi wa mwanzo kufanywa tangu uchaguzi wa rais wa mwaka 2010 uliokuwa na utata, na ambao ulizusha vita na kusababisha watu takribani 3,000 kuuwawa.

Taarifa zaidi kutoka ECOWAS zinasema uchaguzi wa bunge ni hatua muhimu katika ujenzi mpya wa taifa, maendeleo, na kukuza demokrasi nchini Ivory Coast.

-BBC