Irani yatoa USD mil 1.2 kusaidia Kilimo Kwanza


Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Irani imepanga kutoa dola za kimarekani milioni 1.2 (dola milioni 1.2) kuisaidia Tanzania katika utekelezaji wa vitendo kampeni za Kilimo Kwanza.

Taarifa imetolewa leo jijini Dar es Salaam wakati Balozi Msaidizi wa Iran nchini Tanzania Bahman Ahmadi alipotembelea Wizara ya Viwanda na Biashara na kuzungumza na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Lazaro Nyalandu.

Katika mazungumzo hayo yaliyojikita zaidi kuimarisha uhusiano mzuri kibiashara baina
ya nchi hizo mbili, Nyalandu kwa niaba ya Serikali ya Tanzania ameishukuru Iran kwa msaada huo na kuahidi kuwa utatumika kama ulivyokusudiwa.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo amewakaribish Irani yatoa USD mil 1.2 kusaidia Kilimo Kwanza wawekezaji kutoka Iran kuja nchini na kushirikiana na wazalendo katika kutumia vema fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya Kilimo.