KIONGOZI wa chama chenye msimamo wa Kimhafidhina nchini Iran, Hassan Rouhani ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Iran uliofanyika juzi.
Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imesema, Rouhani ameshinda na zaidi ya kura milioni 18, kiwango ambacho ni zaidi ya asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa katika uchaguzi huo.
Wizara hiyo imesema kuwa, idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo walijitokeza kupiga kura kiwango ambacho kinakadiriwa kuwa asilimia sabini na tatu ya watu waliosajiliwa. Mayor wa Mji wa Tehran, Mohamad Baqar Qalibaf ameshika nafasi ya pili baada ya matokeo yote.
-BBC