Insignia Limited Yapata Cheti cha Mazingira cha ISO 14000

Baadhi ya rangi zinazozalishwa na kampuni ya Insignia Limited.

Baadhi ya rangi zinazozalishwa na kampuni ya Insignia Limited.


KAMPUNI inayoongoza kwa uzalishaji wa rangi nchini Tanzania ya Insignia Limited, inajivunia kutangaza kupata cheti cha ISO 14000, cheti cha kiwango cha kimataifa cha uwajibikaji katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira. Viongozi wa kampuni walitangaza mafanikio hayo mjini Dar es Salaam. Cheti hicho cha ISO kilitolewa kuthibitisha viwango vya kampuni kufwatia dhamira yake katika shughuli za utunzaji wa mazingira.

Mwaka 1996, Serikali ya Tanzania ilizindua sera endelevu ya maendeleo ya viwanda (SIDP) (1996-2020) ikiwa na lengo kuu kuchangia mafanikio ya malengo ya muda mrefu kwa maendeleo ya taifa zima kwa ujumla na kuwezesha maendeleo endelevu ya sekta ya viwanda. Moja ya lengo kuu ya sera hiyo ni kuboresha mazingira. Kwa kusukumwa na lengo hili Insignia Ltd. ina Dhamira ya kudumu katika usimamizi na uwajibikaji kwa mazingira.

Kwa mujibu na Bw. Kishan Dhebar, Mkurugenzi mtendaji wa Insignia Ltd, kumekuwa na ongezeko la wananchi wengi hivi sasa kutafuta bidhaa na huduma zinazozingatia uwajibikaji kwa afya na mazingira. Bidhaa ambazo hazita msababishia mtumiaji athari kiafya na mazingira yake pia. Cheti chao kipya cha ISO 14000 kinauhakikishia Umma kuwa kampuni inachukua hatua za tahadhari katika utunzaji wa mazingira, kupitia vifaa vyake vya uendeshaji vinavyofikia viwango vya juu vya mazingira ya ndani ya kiwanda.

“Tunajisikia fahari kusema kuwa kutokana na ithibati hii, vifaa vyote vya Insignia sasa vimethibitishwa kwa kiwango cha kimataifa na ISO 140001. Tunashukuru sana kwa ithibati hii, hata sasa tuna mpango wa hiari wa kufanya zaidi ili kuhifadhi mazingira”. Alieleza Bw. Dhebar.

“Tunafuraha kutangaza ithibati ya ISO 14000 ya vifaa vyetu. Ithibati hii inadhihirisha Dhamira endelevu ya Insignia kwa mazingira na jamii ambamo tunaendesha shughuli zetu. Ithibati ya ISO 14000 inahakikisha kuwa bidhaa zetu zinazalishwa katika hali rafiki kwa mazingira”. Anaongeza.

Insignia Limited ni kampuni inayoifikiria jamii ambapo inaweka kipaumbele katika mfumo wake wa mazingira, ikiwa na matokeo mazuri. “Ni muhimu kwa kila mdau wa kampuni yetu tuweke kiwango cha ubora wa mazingira katika kiwanda. Lengo letu kuu ni kwa mifumo yetu ya ‘kijani’ iwe na matokeo chanya kwa jamii. Kampuni yetu yote, kuanzia viongozi waandamizi hadi mafundi, wanaelewa hili na wanahusika moja kwa moja katika mfumo wa utunzaji mazingira,” anasisitiza Mkurugenzi Mtendaji.

Insignia Limited inaweka sera kali ya mazingira inayohusisha kampuni nzima na kuhakikisha uendeshaji unafanyika katika hali inayopunguzaathari katika mazingira. Ili kuendana na kiwango cha ISO 14000, maeneo muhimu ya sera yanaelezea uzuiaji wa uchafuzi wa mazingira, uboreshaji endelevu wa mfumo usimamizi wa mazingira na kufuatana na mahitaji husika ya kisheria na udhibiti.

Kwa mujibu Meneja Ufundi wa kampuni Bw. Patrick Munguti, ISO 14000 itasaidia Insignia kulinda mazingira, kuzuia uchafuzi na kuboresha utendaji wa kijani. “Insignia ltd tayari imefanya mambo kadhaa ili kulinda mazingira ikiwa ni pamoja na kuzalisha rangi zisizo na risasi, zebaki, arseniki na kromiamu. Cheti cha ISO 14000 kitainua Dhamira yetu ya kuwajibika kwa mazingira”. Anasema.

Insignia imechukua hatua za makusudi katika uwajibikaji wake kwa kuzingatia ulinzi wa mazingira. Kwa kutambua kuwa uhifadhi wa mazingira kwa ujumla ni suala la Dunia nzima, Insignia iliamua kutekeleza shughuli zinazoendelea za utunzaji wa mazingira katika maeneo yake yote ya biashara. Insignia imezingatia zaidi kuzalisha rangi zisizo na madhara kuokoa rasilimali, na kupunguza taka. Shughuli hizi chanya za kampuni zilitambulika na Insignia Limited ikapata cheti cha ISO 14000.

ISO 14000 ni taasisi ya kimataifa ya kujitolea inayoelezea mahitaji ya kuanzisha, kutekeleza na kuendesha mfumo wa usimamizi mazingira (EMS). Kufikia mahitaji ya ISO 14000, kampuni husika ni lazima itekeleze EMS inavyoelezea na kusimamia matokeo ya kampuni kwa mazingira, kupunguza hatari za uchafuzi, kuhakikisha inaendana na kanuni husika na kudhamiria uboreshaji endelevu wa utendaji wake kwa mazingira.

Kuhusu Insignia
Mwaka 1989, Tanzania ilishuhudia kuzaliwa Coral Paints, kampuni ndogo ambayo ingeweza kubadilisha uso wa sekta ya rangi nchini. Ikiendeshwa na dhamira ya kipekee na ubora, kampuni ambayo kwa sasa inajulikana kama Insignia Limited, ilikua kwa kiwango kikubwa na kuvuka mipaka. Hivi leo, Insignia imefikia moja ya malengo yake; ni moja ya kampuni kubwa nchini Tanzania inayoongoza katika utengenezaji wa rangi mbalimbali. Uamuzi wake wa kuleta bidhaa zenye viwango vya hali ya juu nchini Tanzania umewezeshwa na ushirikiano na makampuni makubwa ya kimataifa kama Marmoran (Pty) Ltd, iliyopo Africa ya kusini, Ronseal iliyopo nchini Uingereza na Pat’s Deco ya Ufaransa.

Bidhaa mbili za Coral na Galaxy, zinafafanua ubora wa kampuni ya Insignia. Chini ya majina haya, kampuni inatengeneza rangi na bidhaa nyingine nyingi. Teknolojia ya hali ya juu ipatikanayo katika kampuni hiyo inaipatia kampuni hiyo msaada mkubwa sana katika ushindani. Rangi ya Galaxy inatngenezwa kiufundi, inatumia ujuzi, pembejeo na washauri wa kimataifa, inawapatia wateja wake teknolojia ya kisasa kwenye rangi. Rangi ya Coral paint ni bidhaa inayoongoza katika soko nchini Tanzania. Imepata kibali, na kuimarisha sifa yake kama bidhaa yenye ubora inayoedana na thamani- ya -fedha.

Kiufanisi, miundombinu ya Insignia inajulikana kwa ubora wake. Viwanda vyake vina vifaa vyenye ubora na vya kisasa vinavyotengeneza bidhaa zenye viwango vya kimataifa. Kampuni hii ina viwanda jijini Dar es Salaam, Moshi, Mwanza na Zambia pia ina Vituo vya usambazaji mkoani Moshi, Arusha, Mbeya na Mwanza mikoa mikubwa nchini. Pia kuna uwepo wa mtandao mpana wa wafanyabiashara na malori ya kisasa kuwahakikishia usambazaji wa bidhaa nchini kote. Kampuni hiyo pia ina vituo nchini Rwanda, Burundi na Malawi.