Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya nchi ya India kupitia Benki ya Exim kuikopesha Tanzania sh. bilioni 280 kwa ajili kusaidia kusambaza maji katika Jiji la Dar es Salaam na Mji wa Chalinze. Kulia ni Meneja Mkuu wa Benki ya Exim ya India Geeta Poojary. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa (kushoto) akibadilishana hati ya mkopo wa sh. bilioni 280 kutoka kwa Meneja Mkuu wa Benki ya Exim ya India Geeta Poojary (katikati) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia usambazaji wa huduma za maji kwa Mji wa Chalinze na Jiji la Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa India Debnath Shaw. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es Salaam.