Tata nano, ndio gari lenya bei rahisi sana duniani lakini kulingana na kampeni hiyo, bila shaka kuna uwezekano likawa maarufu zaidi nchini India katika siku chache zijazo.
Dakatri Sitaram Sharma anatazamia kuwa huenda gari hilo likawa kishawishi tosha kwa wakazi wa jimbo la Jhunjunu kujitokeza kufungwa kizazi. Lengo la Daktari Sharma ni kuwa jumla ya wanawake na wanaume elfu 20 watajitokeza kufungwa kizazi.
Kwa taarifa yako, gari sio zawadi tu itakayotolewa kwenye kampeni hiyo. Watakao fika watapewa piki piki, televisheni na vifaa vya kisasa vya kusagia vyakula. Mpango huo hauja lenga tuu wakaazi wa jimbo hilo ambalo mara nyingi linakabiliwa na ukame.
Serikali ya India imekuwa ikitatizika na idadi ya raia wake ambayo inakuwa kwa kasi sana. Hofu za utawala nchini India ni kuwa ifikiapo mwaka wa 2030, heunda idadi ya watu walioko nchini humo ikazidi ile ya wachina.
Hata hivyo hakuna uhakika kuwa kampeni hii itaungwa mkono kote nchini India. Mwaka wa 70 ilipojaribiwa, maelfu ya watu walijotekeza kisha serikali ikashindwa kutimiza ahadi zake kitu kilicho wachukiza wengi ambao walidai kuwa serikali ilikuwa imewalaghai.
CHANZO; BBC Swahili.