“Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na kifo cha ghafla cha Mheshimiwa Clara Mwatuka kwani katika nafasi yake ya Ubunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), alitimiza vyema majukumu yake ya kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Masasi”.
Kutokana na kifo cha Mbunge huyo, Rais Kikwete ametoa pole kwa familia yake kwa kumpoteza Mzazi, kwa chama cha CUF kwa kumpoteza Mwanachama na Mbunge wake, na kwa Wananchi wa Wilaya ya Masasi kwa kumpoteza aliyekuwa Mwakilishi wao Bungeni.
Rais Kikwete amesema anamwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu Clara Mwatuka, na ameiomba familia ya Marehemu kuwa na uvumilivu na utulivu kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya Mzazi na mpendwa wao.