Ikondolelo Lodge Yateuliwa Hoteli Rasmi Mashindano ya Miss Utalii

Mchakato wa uteuzi ulihusisha Hotel zaidi ya saba zilizojitokeza kudhamini fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012. Tanzania itatumia zaidi ya Shilingi za kitanzania Milionimia moja ,ikiwa niudhamini wa gharama za kambi yaWarembo na waandaaji zaidi ya sitini (60) kwamudawa wiki tatu

Hoteli ya kitalii Ikondolelo Lodge iliyoko Kibamba Jijini Dar es salaam ,Imeteuliwa na Bodi ya mashindano ya Miss Utalii Tanzania kuwa Hotel Rasmi ya mashindano hayo Mwaka huu wa 2012.
Mchakato wa uteuzi ulihusisha Hotel zaidi ya saba zilizojitokeza kudhamini fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012. Tanzania itatumia zaidi ya Shilingi za kitanzania Milionimia moja ,ikiwa niudhamini wa gharama za kambi yaWarembo na waandaaji zaidi ya sitini (60) kwamudawa wiki tatu.
Bodi katika kuteua hotel rasmi ya mashindano mwaka huu imezingatia Vigezo vifuatavyo: Usalama wa watu na mali zao, ubora waviwango vya huduma ambayo siyo chini ya hadhi ya nyota (3) , mazingira hotel na utulivu wa eneo husika kulinga na viwango vya kitaifa na Kimataifa vya mashindano ya Miss Utalii, pia kwakuzingatia viwango vilivyowekwa na serikali kupitia Baraza la sanaa la Taifa (BASATA).
Warembo kutoka mikoa yote ya Tanzania na Vyuo vikuu ,wakiwa kambini katika Hotel ya Ikondolelowa tafanya shughuli mbalimbali za maandalizi na za kijamii; zikiwemo , Kujifunza kuogelea katika bwawa lililopo hotelini hapo, Upigaji wa picha za minato katika bustani zinazo zunguka hoteli, watapewa mafunzo maalum ya kutumia maeneo na vifaa mbalimbali vya hotel za kitalii. Aidha washiriki wafainali za taifa za Miss utalii 2012 watapewa mafunzo kuhusiana na utalii, utamaduni, uwekezaji, mazingira, afya ya jamii, elimu ya jamii uzalendo, watafundishwa mbinu za kujieleza, kujiamini na kufanya matangazo.
Mkurugenzi mtendaji wa Ikondolelo Lodge Ndugu Fredy Selekwa ameishukuru Bodi ya Miss utalii Tanzania kwa kuwapa fulsa ya kuwa hotel Rasmi ya Mashindano haya muhimu kwa taifa katika kukuza secta ya utalii na uchumi kwaujumla. Amewahakikishia washiriki na viongozi watakao kuwa kambini kuwapatia huduma zote muhimu kwa kiwango cha kimataifa