IGP Mstaafu Philemoni Mgaya Asherekea Miaka 85

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya.

WAZIRI Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya amewaomba watanzania kuwa na tabia ya utii wa sheria, uaminifu na uadilifu katika nafasi zao wanazozitumukia katika Taifa la Tanzania. Msuya
aliyasema hayo katika sherehe ye kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya iliyofanyika katika Hotel ya Protea, Court Yard jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu alieleza kuwa tabia aliyoionyesha Mgaya wakati wa utumishi wake serikalini inapaswa kuigwa na watanzania wote. “Huyu ndiye Mtanzania halisi aliyelelewa vizuri kuitumikia nchi yake. Hana makuu, ni mkweli na mwadilifu. Akiahidi kufanya jambo fulani analitekeleza bila kuchelewa. Tunahitaji uwajibikaji wa namna hii,” Msuya alisisitiza. 
Alisema kuwa Mgaya alikuwa kiongozi hodari ambaye alisimamia vyema kiapo na kazi zake na
kipindi chake cha uongozi  alikuwa akitoa amri zinatekelezwa mara moja. Naye Mshauri wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited James Rugemalira alitoa wito kwa watanzania kuendele kuunga mkono  jitihada za kuendeleza maeneo mbalimbali ya
kiuchumi ikiwemo viwanda.
Aliwasihi wadau kutoa ushirikiano kwa  kampuni yake inayosambaza bia aina ya Windhoek Larger na Windhoek Draught ambayo inadhamira ya kujenga kiwanda cha kuzalisha bia hizo hapa nchini.
                                       
“Tunatafuta maeneo Kilimanjaro, Tanga na Bukoba ili tuweze kujenga kiwanda hapa nchini.
Tumedhamilia kufanya hivyo na tutafanya,” Rugemalira alisisitiza.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira aliwashukuru wananchi kwa
kukubali kujumuika pamoja katika hafla hiyo na kumwomba Mzee Mgaya aendelee kuwapa
mwongozo wa namna ya kuenenda katika maisha. 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa aliwaomba watanzania kuwa na moyo wa unyenyekevu na kujitolea kulitumikia taifa katika utumishi wao kama ilivyokuwa kwa IGP mstaaafu Mzee Mgaya.
Wageni wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri wa Habari na Utangazaji Fenera Mukangara, Katibu Mkuu Msaaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Bakari Mwapachu, Balozi Antoni
Nyaki na wazee wengine maarufu kama Timothy Msangi.

 Mara Baada ya Ibada katika Kanisa la Azania Front wakati wa  kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya.
Baadhi ya waumini mbalimbali wakiwa nje baada ya Ibada  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Mstaafu Philemoni Mgaya akiwa katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
 Keki
Waziri  Mkuu
Mstaafu Cleopa Msuya akimpongeza aliyekuwa IGP Philemoni Mgaya
 Mzee Timothy Msangi akieleza Historia fupi ya IGP Mstaafu Philemoni Msangi
 Askofu Mkuu
wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa akitoa salam za Pongezi kwa IGP mstaafu
 Mshauri
wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited
James Rugemalira akitoa pongezi zake kwa IGP Mstaafu na kuelezea 
Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited
 Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira akitoa salam za Pongezi kwa IGP mstaafu

Mshereheshaji Joe Mgaya ambaye ni Mtoto wa IGP Mstaafu Philemoni Mgaya akisherehesha
 Waziri wa Habari na Utangazaji Fenera Mukangara  akimpa mkono wa Pongezi IGP mstaafu
 
 Wakiwa katika Furaha
IGP Mstaafu akipokea zawadi

IGP Mstaafu Philemoni Mgaya akikata keki huku amezungukwa na wajukuu wake
 Watu mbalimbali wakiwa katika Sherehe hiyo
 Burudani ya nguvu