Na Ally Daud-MAELEZO
Jopo la Elimu ya Kiislamu nchini (IEP) limetangaza matokeo ya wanafunzi waliofanya mtihani wa dini hiyo wa kuhitimu darasa la saba Agosti 12 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mwandamizi wa jopo hilo Bw. Suleimani Daud alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Bw. Suleimani amesema kuwa wanafunzi ambao walifanya mtihani huo idadi yao ilikuwa 86,613 kati ya wanafunzi 93,101 waliojisajili nchini kutoka shule 3094 ambazo wanafunzi walifanya mtihani huo mwaka 2015 zaidi ya wanafunzi 2559 kutoka shule mwaka 2014.
Idadi za hiyo ya wanafunzi imeongezeka kutokana na ongezeko la wilaya zilizoshiriki katika mtihani huo kutoka Wilaya 115 kwa mwaka 2014 hadi kufikia Wilaya 127 mwaka huu ambazo ni sawa na asilimia 10.4.
Aidha Bw. Daud amesema kuwa kiwango cha ufaulu kimepungua kutoka wastani wa 46.45 mwaka jana hadi kufikia wastani wa 40.1 sawa na asilimia 13.67 mwa huu.
Mtihani ulikuwa na jumla ya alama asilimia 100 wastani wa ufaulu kitaifa ni asilimia 13.67 ambao umepatikana kwa kutafuta wastani huo wa kila mkoa na kugawa kwa idadi ya mikoa yote nchini.