IBF Yaleta Hamasa Namibia

Mpambano wa kutafuta Mfalme wa uzito wa Bantam wa Kimataifa (IBF International Bantamweight Title) kati ya mabondia Immaneul Naidjala a.ka. Prince kutoka nchini Namibia and bondia mwenzake Lesley Sekotswe kutoka nchini Botswana umeanza kuleta hamasha kubwa katika nchi hii yenye wakazi wapatao milioni mbili.

Mpambano wa kutafuta Mfalme wa uzito wa Bantam wa Kimataifa (IBF International Bantamweight Title) kati ya mabondia Immaneul Naidjala a.ka. Prince kutoka nchini Namibia and bondia mwenzake Lesley Sekotswe kutoka nchini Botswana umeanza kuleta hamasha kubwa katika nchi hii yenye wakazi wapatao milioni mbili.

Mabondia wote wawili walikutana kwa mara nyingine tena leo katika ofisi za Bodi ya Mieleka na Ngumi ya Namibia katika zoezi la kupima uzito na ilibidi askari zaidi ya 15 kuwazuia wasizipige kavukavu.

Moto ulianza kuwashwa wakati bondia Lesley Sekotswe wa Botswana alipoingia katika chumba cha waandishi wa habari na kutangaza rasmi kuwa atamshughulikia Prince Immanuel Naidjala vilivyo na asijaribu kufikiri kuwa atafika zaidi ya raundi ya tatu.

Wakati huo Prince Immanuel alikuwa kwenye chumba cha kupimia afya za wabondia na alikurupuka kutaka kumwingilia Lesley kabla ya askari waliokodishwa na Promota Nestor Tobias kuingilia kati na kuwatenganisha ili wasianze mpambano unaosubiriwa kesho.

Katika zoezi la vipimo ambalo lilisimamiwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi, bondia Lesely Sekotswe wa Botswana alikutwa na kilo 53.45 wakati Prince Immanuel wa Namibia alikutwa na kilo 53.35. Rais Ngowi aliwatangaza mabondia wote kuwa katika uzito unaotakiwa.

Daktari Leonardo Perves kutoka nchini Cuba inayojulikana kwa kutoa mabondia wengi mabingwa wa mashindano ya Olimpiki na Dunia ndiye aliyewapima mabondia hao na kuwatangaza kuwa wana afya nzuri ya kuweza kuzipiga.

Mpambano huu utafanyika siku moja kabla ya sherehe za uhuru wa nchi ya Namibia katika ukumbi wa Windhoek Country Club Resort and Casino ulioko nje kidogo mwa jiji la Windhoek na utatanguliwa na mepambano mengine kadhaa ya utangulizi.

Katika mkutano na waandishi wa bahari Rais Ngowi aliisifu serikali ya nchi ya Namibia kwa jinsi inavyoipa kipa umbele tasnia ya ngumi katika juhudi zake za kuitangaza nchi na kujenga ajira kwa vijana. Ngowi aliihakikishia nchi ya Namibia kuwa ataiingiza katika programu ya IBF ya Utalii wa Michezo (IBF Sports Tourism) ili nayo iweze kufaidi katika maendeleo ya Utalii wa Michezo duniani.