Mshindi wa jumla wa mashindano ya kuwania kombe la Johnnie Walker Waitara 2012 Sudson Manatsa akinyanyua juu vikombe vyake viwili alivyoshinda wakati wa Mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Gofu Lugalo jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake kikali cha Johnnie Walker.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Stephen Gannon akimkabidhi zawadi Mshindi wa pili wa daraja A, Aidan Nziku kikombe na zawadi nyingine baada ya kuibuka mshindi wa kundi hilo katika mashindano ya kuwania kombe la Johnnie Walker Waitara 2012. Kampuni ya Bia ya Serengeti imedhamini mashindano hayo kupitia kinywaji chake cha Johnnie Walker.
Mshindi mwingine (kushoto) akikabidhiwa kombe na zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Stephen Gannon