HABARI za jioni mabibi na mabwana, Itifaki imezingatiwa.
Ni furaha ya pekee na heshima kubwa waliyonipa Oriflame Tanzania kwa kunikaribisha kwenye uzinduzi wa katalog yao ya mwezi Julai hadi Septemba.
Binafsi, napenda kuipongeza kampuni ya Oriflame yenye makao yake makuu nchini Sweden, kwa kuthamini ubora wa ngozi za watanzania na kuamua kuwaletea bidhaa ambazo zimetengenezwa na malighafi za asili zikiwemo matunda, maua na mimea mingine.
Leo hii wanazindua katalog ambayo imeongezwa bidhaa mpya na bora zaidi kama vile manukato, mafuta na vipodozi vitakavyoweza kuisaidia ngozi yako kuwa na afya na yenye mvuto wakati wote.
Vilevile napenda kutambua fursa ambazo Oriflame imetoa katika kuinua uchumi wa taifa letu. Wametambua uwezo wa watanzania katika kujishughulisha na biashara na hivyo kuwapatia nafasi hususan kina mama na kina dada ya kujiendeleza kuichumi kwa kuwa washauri na wasambazaji wa bidhaa mbalimbali za Oriflame.
Biashara inayohusiana na urembo siyo kwa akina mama na kina dada pekee hata kina kaka na kina baba pia wanaweza kufanya kwani bidhaa hizi ni kwa watumiaji wote wa kike na wa kiume, hivyo napendekeza wenzetu wajiunge kwa wingi pia.
Watu wengi wamekuwa wakiona kuwa hii ni namna ya umachinga kutokana na uhitaji wa kuzunguka huku na kule kutafuta wateja na kushawishi watu kujiunga kununua bidhaa zenu. Ila mimi nasema tukumbuke msemo wa “mchumia juani hulia kivulini” na kivuli cha biashara hii ni kuwa kamwe haitorudi nyuma endapo unajibidiisha.
Mwisho napenda niwapongeze washauri na wasambazaji wa Oriflame pamoja na wafanyakazi wote kwa kuendelea kujituma katika kila hali pasipo kukata tamaa kwani wao ndio chachu ya kampuni hii kufikia hapa ilipo.
Kama ambavyo kampuni ya Oriflame inasimamia watu kuwa na Umoja, Ari na Shauku katika utendaji wa kazi, nami nasisitiza wanachama wa Oriflame pamoja na wananchi wote kwa ujumla kuwa na Umoja, Ari and Shauku katika kufanya kazi. Hii ndio njia pekee itakayoweza kuleta maendeleo kwa haraka katika taifa letu.
Na kwa kusema haya napenda kuzindua rasmi katalog hii maalum kwa mwezi Julai hadi Septemba 2012.
Asanteni sana.