Hoteli ya Kisasa ya Shangani Yazinduliwa Mkoani Mtwara

Mandhari ya nje ya Hoteli ya Kisasa ya Shangani Hotel Apartments iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego usiku jana mjini Mtwara. Pia ulizinduliwa Mgahawa wa kisasa ambapo wageni waalikwa walifaidi kula chakula cha usiku kilichopikwa na wapishi waliobobea kwa mapishi yenye vionjo vya kila aina.

Akida Zidikheri (kushoto) mmiliki wa Shangani Hotel Apartments na . Said Aboud (kulia)pamoja na Mstahiki Mayor wa Manispaa ya Mtwara, Selemani Mtalika ndani ya mgahawa huo wa kisasa uliopo katika hoteli hiyo.

Mmiliki wa Shangani Hotel Apartments, Akida Zidikheri wakiwa ndani ya moja ya Apartments pamoja naMkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego (kulia), na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara  Fatma S. Ally (kushoto).

Mmiliki wa Shangani Hotel Apartments, Akida Zidikheri akiwaonesha wageni waalikwa sehemu ya kutengenezea mikate (bakery), iliyomo kwenye jiko la mgahawa huo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara, Seleman Mtalika akimkaribisha mkuu wa Wilaya ili aweze kumkaribisha rasmi Mkuu wa Mkoa ili azungumze na wageni waalikwa.

Mmiliki wa Shangani Hotel Apartments, Akida Zidikheri akitoa shukrani kwa wageni waalikwa waliohudhuria ufunguzi huo.

Wakipata mlo wa usiku kwenye mgahawa huo, kutoka kushoto ni;Mstahiki Mayor wa Manispaa ya Mtwara, Selemani Mtalika, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego Mwajuma Mchuka Station Manager wa ATC Mtwarana.

Ni kula kwa kwenda mbele