UMAKINI kwa mara nyingine tena umewekwa katika uhitaji wa wataalamu zaidi na kuboresha miundombinu ndani ya sekta ya utabibu wa upasuaji wa mfumo wa fahamu. Hii inakuja baada ya ziara ya hivi karibuni na timu ya madaktari kutoka hospitali ya Apollo nchini India.
Madaktari ambao walikuwa nchini kwa lengo la kujenga uhusiano unaoendelea kati ya hospitali hiyo na Tanzania, walipata fursa ya kutembelea taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na maboresho ya ujuzi wa wauguzi ambao walipata mafunzo kutoka hospitali ya Apollo.
Matibabu ya magonjwa ya mfumo wa fahamu ni mada nyeti yenye matatizo mbalimbali kama yakifanyika kwa namna isiyo sahihi. Kuvurigika kwa mishipa ya fahamu ni ugonjwa ambao unatokea katikati na pembeni ya mfumo wa neva. Ambapo kimuundo, upungufu wa bio-kemikali au umeme kutokuwa sawa katika ubongo, uti wa mgongo au mishipa mingine na inaweza kusababisha dalili za aina mbalimbali.
Tanzania kwa sasa kuna madaktari wa mfumo wa fahamu 7 jumla ambao wote kwa sasa ni watendaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam. Aidha tofauti wenzao wa nchini India ukosefu wa data za kutosha kunamaanisha haiwezekani kuwa na muonekano sahihi wa madhara ya maradhi ya mishipa ya fahamu kwa Watanzania kwa ujumla.
Akizungumzia hili daktari Profesa Krishna Kambadoor Mkurugenzi wa Taasisi ya sayansi ya mfumo wa fahamu kutoka Hospitali ya Apollo ya Bangalore alisema kuwa hali ya sasa inaweza kukadiriwa kutoka takwimu za India na kujifunza. Kulingana na nguvu ya idadi ya watu na mfanano wa magonjwa ya India na Tanzania (ukiondoa magonjwa ya kuambukiza) mfano unaweza kupatikana.
Baada ya kuthibitisha na watendaji wa Tanzania Prof. Krishna alikuwa na uwezo wa kuonyesha mambo mawili ambayo ni ya muhimu kuyatazama kwa ajili ya baadaye, haya ni tabia za ulaji za watu pamoja na ongezeko la umri wa kuishi wa watu kwa ujumla. Mlo usio kamili husababisha kesi nyingi za magonjwa ya kisukari na matatizo yanayoambatana katika sehemu za mwili ikiwa ni pamoja na kupoteza ufahamu (neurocognitive dysfunctions).
Ambapo tunaweza kuipongeza sekta yetu ya afya kwa ongezeko la hivi karibuni la umri wa kuishi ni lazima pia kuangalia upande wa pili wa sarafu na kushughulikia matatizo mbalimbali ambayo ni uhakika wa kufanya madhara. Matatizo haya ni pamoja na kuongezeka idadi ya magonjwa yanayohusiana na umri mkubwa miongoni mwao yakiwemo, mishipa ya fahamu na moyo kwa ujumla.
Ujio wa madaktari pia ulikuwa sehemu ya mipango ya Apollo ya uliotazamiwa katika kuendeleza sekta ya sayansi ya mfumo wa fahamu Tanzania. Hii ni hatua ambayo itatazama utengenezaji wa vituo mtaalamu ambapo ita boresha huduma na kuongeza wataalamu wa afya hapa nchini. Hospitali za Apollo zinatazamia kuleta zaidi ya miaka 20 ya maendeleo ya teknolojia na Prof. Krishna anasema kuwa “India kama Tanzania ilikuwa katika hali kama hii miongo 3 iliyopita na tangu wakati imeingia kutoka taifa linaloendelea na kuwa karibu sawa na taifa lililoendelea”.
Anasisitiza kuwa “kwa juhudi za pamoja kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi binafsi na serikali basi Tanzania kwa upande wa matibabu inaweza kufikia ukuaji ulioonekana India kwa miaka 20 na zaidi, katika muda wa miaka 5”.
Uhusiano kati ya hospitali za Apollo na Tanzania umekuwa na matunda kwa muda mfupi wa muongo mmoja. Mipango inayopendekezwa itakuwa muhimu katika maendeleo ya miundombinu ya sekta ya afya. “kwa kuwa huduma za afya si kama huduma za gari ambapo baada ya uchunguzi yanaachiwa tu, upatikanaji wa teknolojia ya kisasa na utaalamu utahakikisha uwepo na kuendelea kwa mchakato wa huduma ajili ya wagonjwa” alihitimisha Prof. Krishna.
Katika siku chache zijazo hospitali za Apollo zina mipango ya kambi ya matibabu mwisho wa mwezi wa Machi, hii itaruhusu watu kuwaona madaktari kwa ushauri juu ya maradhi mbalimbali. Kazi ambayo ipo katika hatua za kukamilika itakuwa pia kama jukwaa kwa ajili ya kukusanya data ambazo zitatoa picha ya hali ya sasa ya magonjwa yanayohusiana na mishipa ya fahamu ndani ya nchi.
Kuhusu Hospitali za Apollo
Idara ya Magonjwa ya mfumo wa fahamu ya Hospitali ya Apollo inawekwa kati ya hospitali bora katika nchi. Wigo wa idara hii ni pamoja na uchunguzi na matibabu ya magonjwa yanayoathiri ubongo, uti wa mgongo, misuli na mishipa ya fahamu.
Uchunguzi wote wa magonjwa haya ujulikanao kitaalamu kama “EEG”, “video telemetry”, “electromyography”, “stimulators magnetic” na vichochea uwezo vinapatikana katika vituo hivi. Vifaa hivyo ni pamoja na “MRI Scan” na “MR angiography”, “CT Scan” ya mfumo wa fahamu, “angiography” na “SPECT” ya kawaida.
Vidonge tiba kwa wagonjwa wa kiharusi na “botulinum toxin therapy” kwa ”focal dystopia” hutumiwa na madaktari wakati muhimu. Wapasuaji wa mfumo wa fahamu mara kwa mara hufanya upasuaji wa kichwani na mgongoni, “stereotactic” bayopsi ya uvimbe “deep-seated” na “stereotactic radio surgery” kwa ajili ya matibabu ya ulemavu “artereovenous” na uvimbe. “Aneurysms”, ulemavu wa mishipa na kichwa & shingo fuvu upasuaji wake pia hufanyika katika hospitali ya Apollo.