Hospitali za Apollo Kuokoa Zaidi ya Watu 100 Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar

Hospitali za Apollo Kuokoa Zaidi ya Watu 100 Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam
Hospitali za Apollo Kuokoa Zaidi ya Watu 100 Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam
HOSPITALI za Apollo zimekuwa mstari wa mbele kwa teknolojia ya hali ya juu na zinaongoza katika kutoa huduma nafuu za matibabu kwa wagonjwa duniani kote. Apollo wanashiriki kwenye Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwa mara ya kwanza.

Hospitali za Apollo ziko hapa kutangaza huduma wanazotoa na kuongeza uelewa kuhusu Apollo. Wageni mbalimbali wanaotembelea Saba Saba wanaweza sasa kuelimishwa kuhusu huduma mbalimbali na teknolojia zinazotolewa na Hospitali za Apollo kama vile Upasuaji wa Kiroboti, na nyingine zijulikanazo kitaalamu kama ‘Noralis Tx’, ‘PET MRI’ na ‘CyberKnife’ hizo ni baadhi tu. Teknolojia hizi mpya zinasaidia ufanisi katika uchunguzi/ugunduzi hivyo kuboresha matibabu anayoyapata mgonjwa. Teknolojia hizi pia zimeruhusu Hospitali za Apollo kuwa za kwanza kufanya upasuaji mara nyingi zaidi India na duniani kote. Mfano mzuri wa moja ya upasuaji uliofanikiwa sana huko India ulikuwa ule wa kurekebisha tatizo la uti wa mgongo la kuzaliwa kwa mtoto wa miaka 6 Mtanzania kwa kutumia pingili za kurudishia.

Ndugu Paras Duggal Meneja Masoko Mwandamizi wa Hospitali za Apollo New Delhi, India anatoa wito kwa watu wanaohitaji kupata ushauri zaidi juu ya ripoti zao za matibabu. Anasema kuwa ripoti hizi sasa zinaweza kutumwa kwa barua pepe inayotolewa kwenye maonyesho ya Saba Saba. Ripoti hizi zitapelekwa kwa madaktari na wataalamu ambao watatoa ushauri wao wa kitaalamu juu ya nini cha kufanya. Pia anatoa wito kwa wageni ambao wanahitaji kwenda India kwa ajili ya matibabu kutumia fursa hii.

Balozi wa India Shri Debnath Shaw alipotembelea banda la Hospitali ya Apollo alisifu juhudi zilizokwa na Hospitali za Apollo katika kukuza uelewa na kuelimisha jamii ya Watanzania kwa kuzingatia huduma za afya zinazotolewa na Hospitali za Apollo.

Tangu kufunguliwa kwa maonyesho haya na Mheshimiwa Jakaya Kikwete, Ndg. Duggai amepata zaidi ya wageni mia moja katika banda la Hospitali za Apollo. Maswali ya wengi yamekuwa kutaka kufahamu juu ya gharama za matibabu, aina ya matibabu yanayotolewa na Hospitali za Apollo na nini mtu atarajie anapotembelea Hospitali za Apollo. Hata hivyo watu wengi, wamekuwa wakiuliza kuhusu ushauri na maoni ya zaidi kuhusu hali za afya zao au wanafamilia na ndugu zao.

Bi. Angel Kessy ni mfano wa wanawake waliotembelea banda hili wakiulizia ushauri wa matibabu kwa ajili ya mama yake. Mama yake amekuwa akiugua maumivu ya mgongo na uti wa mgongo kwa miaka mingi, baada ya mjadala mfupi alishauriwa kutuma ripoti yake ya matibabu kwa barua pepe ambazo zitatumwa kwa mtaalamu. Bw. Charles Abel na Bibi. Nesta Mwingizo pia ni mfano wa watu ambao maswali yao yalijibiwa.

Hospitali za Apollo zimekuwa zikitambulika kwenda mbali zaidi kuwafanya wagonjwa wao wajisikie vizuri. Wanawasaidia wagonjwa na waangalizi wao kwa umakini zaidi wa huduma ambazo ni bora Wageni wanahimizwa kuleta ripoti zao za matibabu kwenye banda hili. Hata hivyo, Ndg. Duggai pia yuko tayari kupokea ripoti kupitia barua pepe. Kisha ataipeleka ripoti hiyo kwa mtaalamu husika. Tutumie fursa hii adimu.