Hongereni akinamama Tanzania na duniani kote

Mama Mecktilda Lutabana Mushi, akiwawakilisha akinamama wote Tanzania na ulimwenguni kupokea salamu za pongezi kwa kuadhimisha Siku ya Mama Duniani, 13, 2012.

KWA kutambua mchango na kazi kubwa ya akina mama wote nchini Tanzania, na popote ulimwenguni natumia nafasi hii kumpongeza mama yangu Mecktilda Lutabana Mushi kwa kuadhimisha Siku ya Mama Duniani.

Waungwana na wazalendo popote ulimwenguni tunatambua kazi kubwa mnayoifanya ya kuijenga jamii kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa kulingana na shughuli mbalimbali mnazozifanya kwa kila mmoja na nafasi yake.

Tutaendelea kuwajali ikiwa ni pamoja na kutambua mchango mkubwa ulioutoa na mnaoendelea kuutoa katika ujenzi wa jamii na hatimaye taifa kwa jumla. Mungu aendelee kuwalinda popote mlipo na kwa kila mlifanyalo kwa mapenzi mema juu ya familia zenu.
Mungu wabariki akinamama Tanzania na Mungu wabariki akinamama ulimwenguni.