Hofu Magaidi; Wapiga Bomu Kijijini Morogoro, Wanne Wajeruhiwa

Baadhi ya askari wa FFU wakiwa eneo lilipotupwa bomu.

Baadhi ya askari wa FFU wakiwa eneo lilipotupwa bomu.

Gari aina ya Nissan Patrol namba za usajili SM 10632 mali ya Serikali za Mitaa iliyoharibiwa na bomu lililotupwa.

Gari aina ya Nissan Patrol namba za usajili SM 10632 mali ya Serikali za Mitaa iliyoharibiwa na bomu lililotupwa.

Baadhi ya wanahabari waliotembelea eneo hilo la tukio wakipata taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo la mlipuko wa bomu.

Baadhi ya wanahabari waliotembelea eneo hilo la tukio wakipata taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo la mlipuko wa bomu.

Picha inayoonesha madhara ya bomu hilo lililotupwa.

Picha inayoonesha madhara ya bomu hilo lililotupwa.

Picha inayoonesha madhara ya bomu hilo lililotupwa.

Picha inayoonesha madhara ya bomu hilo lililotupwa.

Picha inayoonesha madhara ya bomu hilo lililotupwa.

Picha inayoonesha madhara ya bomu hilo lililotupwa.


Na Joachim Mushi, Ifakara

HOFU ya watu wanaodhaniwa kuwa magaidi imetanda katika Kijiji cha Msolwa Ujamaa, kilichopo Wilaya ya Morogoro Vijijini baada ya watu wawili kupiga bomu la kutupa kwa mkono katika kijiji hicho na kujeruhi vibaya watu wanne waliokuwa wakiwadhibiti watu hao.

Akizungumzia jana na dev.kisakuzi.com eneo la tukio mmoja wa wanakijiji aliyeshuhudia tukio hilo, Ibrahim Ally mkazi wa Kijiji cha Msolwa Ujamaa alisema watu hao wanaodhaniwa kuwa magaidi walimkodi mwendesha pikipiki wa kijijini hapo na waliomba wapelekwe Kijiji cha jirani wakiwa safarini mazungumzo ya watu hao yalimwogofya dereva bodaboda na kuanza kuwashuku.

Baada ya hapo aliwaambia yeye alikuwa na njaa hivyo aliwaomba wasimame na kula chipsi kidogo kisha waendelee na safari yao, wakiwa eneo walilosimama dereva wa bodaboda alikwenda kwa siri na kuwajulisha baadhi ya jamaa zake kuwa anaabiria ambao wamemkodi lakini hawaelewi hivyo anaomba wawahoji ili kuwajua kiundani.

Ndipo walipokwenda kudi la watu watano na kuanza kuwahoji jamaa hao na baada ya kujikanyaga walikubaliana wawapeleke kwa Mtendaji wa Kijiji kwa mahojiano zaidi, wakiwa njiani karibu na ofisi ya CCM kijijini hapo mmoja wa watu hao alijaribu kuwakimbia ndipo walipoanza kumfukuza huku wengine wakimdhibiti mwenzake.

Ally alisema kijana aliyebakia baada ya kudhibitiwa akiwa amelala chini alitoa kitu kinachodhaniwa kuwa bomu na kukitupa chini ndipo uliposikika mlipuko mkubwa mithili ya bomu kijijini hapo ambao uliwajeruhi vibaya watu watano waliokuwa eneo la purukushani hiyo.

“…baada ya kishindo hicho majeruhi wote watano walijikuta wameanguka chini na kubaki kimya kidogo kisha tukaanza kusikia mayowe ya wao kuomba msaada…nakufa nisaidieni…walikuwa wakiita huku wakiwa wamelalachini lakini hakuna aliyesogea kila mtu alikuwa akikimbia kuhofia kishindo hicho. Anasema baadhi yao baadaye walipata nguvu na kuinuka na kuanza kutimua mbio huku wakiomba msaada,” alisema Ally.

Wanakijiji hao walisema waliojeruhiwa ni dereva wa gari la diwani ambaye akikuja kutokea Ifakara kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi ambaye amejeruhiwa begani na mguuni, mwalimu toka Shule ya Msingi Sanje, Amos Msokole pamoja na Mzee mmoja aliyekuwa akisaidia kuwadhibidi watu hao ambaye amevunjika miguu yote na mkono.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia gari aina ya Toyota Rand Cruise iliyokuwa ikitumiwa na diwani aliyefika kijijini hapo kuhudhuria sherehe za Mei Mosi katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM), kijijini hapo liki limevunjwa vioo vya upande mmoja na kutobolewa mithili limepigwa risasi na kutoboa matundu kwenye bodi karibu na mlango wa mbele wa gari hiyo, mlipuko huwo pia umetoboa baadhi ya mabati ya nyumba za jirani na eneo ulipotokea.

“…Sisi tunahisi hawa ni watu wa kujitoa muhanga, na tumekuwa tukisikia wapo juu ya milimani huko wanafanya mazoezi yao huko milimani na hivi karibuni walikamatwa wengine Kidatu,” alisema mmoja wa wanakijiji hicho.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia askari wa kikosi cha FFU wakiwa na silaha wamelizunguka eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi, akiwemo Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ambaye alisema uchunguzi zaidi unafanywa juu ya tukio hilo.