SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) kwa kushilikiana na Shirika la kisukari kimataifa la International Diabetes Federation (IDF) walianzisha Siku ya Kisukari Duniani mnamo mwaka 1991 ili kuadhimisha kuzaliwa kwa mwanasayansi Frederick Banting ambaye kwa kushirikiana na Charles Best aligundua tiba muhimu kwa wagonjwa wa kisukari ya insulin mnamo mwaka 1922.
Novemba 14 Kila mwaka mashirika ya kiserikali, mashirika binafsi, wagonjwa wakisukari na wadau mbalimbali hukutana ili kuadhimisha siku hii duniani kote. Siku hiyo huadhimishwa kwa kaulimbiu mbalimbali, kampeni na pia hutoa nafasi kwa wagonjwa wa kisukari na wasio wagonjwa kufanya vipimo na mashauriano na wataalamu na madaktari wa ugonjwa wa kisukari. Mwaka huu kauli mbiuni Go Blue for Breakfast kauli mbiu hiyo inasisitiza ulaji wa afya wa kifungua kinywa.
Kisukari ni ugonjwa wenye matibabu ya muda mrefu unaosababishwa na hitilafu kwenye mmeng’enyo wa chakula ndani ya mwili wa binadamu unaoambatana na kiasi cha juu cha sukari kwenye mzunguko wa damu. Hali kadhalika, hutokana kongosho kutengeneza kiasi kidogo cha insulini au seli za mwili kushindwa kufanyia kazi insulin inayotegenezwa na kongosho.
Mathalan, kuna aina mbili za ugonjwa wa kisukari ikiwemo aina ya kwanza ya kisukari ambayo husababishwa na mwili kushindwa kutengeneza insulin yakutosha ambayo chanzo chake hakiko bayana. Aina ya pili ya kisukari yenyewe husababishwa na seli za mwili kushindwa kufanyia kazi insulin inayotengenezwa mwilini ambayo chanzo chake kikubwa ni ukosefu wa mazoezi ya mwili na kuwa na uzito kupindukia.
Kauli mbiu ya mwaka huu inatilia mkazo umuhimu kupata chakula bora hususan katika kifunguwa kinywa ili kuepuka aina ya pili ya kisukari na matatizo yanatokanayo na aina hiyo ya kisukari. Jambo ambalo litasaidia jamii kuweka uzito waokatika kiasi kinachotakiwa nakuweka kiasi chao cha sukari mwilini katika kiwango salama pia.
Shirika la afyadunia – WHO linakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 180 duniani wana ungonjwa wa kisukari. Ambapo, inakadiriwa pia kufikia mwaka 2030 idadi hiyo itakuwa imeongezeka mara mbili zaidi kama hakutakuwa najitihada madhubuti dhidi ya ugonjwa huo. Katika mwaka 2005 inakadiriwa watu milioni 1.1 walifariki kutokana naugonjwawa kisukari ikiwa asilimia 80 ya vifo hivyo vikitokea katika nchi zenye kipato cha chini na kati katika watu walio na umri chini ya miaka 70. Hali kadhalika, asilimia 55 ya vifo hivyo viliripotiwa kutokea kwa wanawake (i).
Kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la afya la kimataifa la International Diabetes Federation (IDF), katika mwaka 2012, idadi ya watu waliogundulika na ugonjwa wa kisukari nchini Tanzania inakidiriwa kuwa nusu ya milioni ambapo watu milioni 1.4 wakiwa hawajafanyiwa uchunguzi sahihi. Hali kadhalika, asilimia 50 ya watu wanaoishi na aina ya pili ya kisukari nchini Tanzania hawa nauelewa wa juu ya hali zao za afya.
Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi zinazoendelea, inakabiliwa nachanga moto kwenye masuala ya afya hususan magonjwa sugu ikiwemo ugonjwa wa kisukari. Suala ambalo linakwamisha na kuzorotesha uchumi wataifa na maendeleo kwa ujumla. Inakisiwa bilioni 2.8 za dola ya Kimarekani hutumika barani Afrika katika kukabilia na na magonjwa mbalimbali sugu (iii).
India ni miongoni mwa nchi zinazoendelea lakini. Pia ni moja wapo ya nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi kubwa zaidi duniani. Na mikakati yake yakupiga na dhidi ya ugonjwa wa kisukari ni mfano mzuri kwa nchi kama Tanzania na wakuigwa.
Hivi karibuni Hospitali za Apollo ziliungana na shirika mashuhuri la dawa an afya la Sanofi ili kutoa huduma za afya kwa wagonjwa wa kisukari kupitia kliniki za kisukari. Dhum uni lao likiwa kuanzisha kliniki 50 kufikia mwishoni mwa mwaka 2014 anasemaPrathap Reddy, Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo, akiongeza kuwa kliniki nyingine 100 zitajengwa mwakani.
Kupitia ushirikiano huo Apollo na Sanofi watahudumia waongjwa wa kisukari na kuwezesha upatikanaji wa elimu, vifaa, matibabu na uwanagalizi wa karibu kwa wagonjwa kupitia uzoefu na utalaamu wa mashirika hao gwiji wa afya. Uamuzi huu ni kwa ajili ya kukabilia na na ongezeko la wagonjwa wanaogundulika na kisukari nchini India na duniani.
Zaidi katika utoaji wa huduma katika kliniki hizo, aina ya huduma zitakazotolewa zitakuwa za kitaalamu, za kisasa na uangalizi wa hali ya juu zitakazohusishwa wagonjwa wake wa kisukari na pia mienendo ya maisha ya wagonjwa hao. Kliniki hizo pia zinatilia mkazo zaidi kinga dhidi ya kisukari, matibabu ya mapema kwa wagonjwa wa kisukari ili kuzuia matatizo makubwa zaidi.
Tunapoelekea kwenye kilele cha siku ya kisukari duniani, ni budi kuelewa kwamba bado tuko nyuma kufikia ushindi kwenye vita zidi ya ugonjwa wa kisukari. Lipo tumaini kwa ndugu, jamaa na marafiki zetu ambao wanasumbuliwa na kisukali endapo kliniki za kisukari zitajengwa kwa wingi zaidi nchini Tanzania. Kama nchi shirika ya India ambayo inasadikika kuwa na usambaaji mkubwa wa ugonjwa wa kisukari, ambapo Apollo imechukua jukumu la kujenga kliniki za kisukari 50 ikishirikia na Sanofi na pia ni mashirika yaliyotambuliwa na shirika la Kisukari la nchini marekani American Diabetes Association kwa huduma zake mbadala katika masuala ya kisukari.
Tanzania inahitaji kliniki kama hizi kutokana na ukweli kuwa huduma kwa wagonjwa wa kisukari bado ziko nyuma pamoja na uelewa mdogowawatanzaniakuhusuugonjwawakisukari. Uwepo wa kliniki kama hizi kutasaidia kuleta uwelewa ikiwa na pamoja ya jinsi ya kujikinga na ugonjwa huomba lina wagonjwa kupata matibabu yanayostahili.
Kliniki za kisukari zimeundwa kusaidia watu walio katika hatari ya kupata kisukari na hawa nau fahamu juu ya afya au hali zao zinalenga pia kutoa tiba mbadala na mahususi kupitia vipimo vinavyoshiria kama mtu yuko katika hatua za mwanzo za ugonjwa. Kiliniki hizo hutoa ushauri juu ya mlo kamili na maisha kwa ujumla ili kuepukana na kisukari.
Wagonjwa wa kiuskari wata kuwa na nafasi kubwa ya kuepuka matatizo na maradhi yatokanayo na ugonjwa wa kisukari yakiwemo maradhi ya moyo, matatizo ya ubongo, kushindwa kwa figo, upofu, kukosa nguvu za kiume na upotevu wabaadhi ya viungo vya mwili hususan miguu na vidole.
Mbali na kuanzisha kliniki zaidi za kisukari, habari njema ni kuwa watanzania bado wanauwezoa wa kuepuka maradhi yatokanayo na kisukari kwa kuendesha maisha salama kupata chakula bora kama inavyoashiria kauli mbiu ya mwaka huu ya “go blue for breakfast”.
Zaidi kuhusu hospitali za apollo
Hospitali ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo “Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika elimu na utafiti kwa ajili ya jamii ya kibinadamu”.
Katika miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini India.
Hospitali za Apollo zimekuwa mstari wa mbele katika kuleta mapinduzi ya sekta ya afya nchini india ikiwa na vitanda 10,000 katika hospitali zake 61 kote nchini india, Asia na Africa. Maduka ya madawa 1,600, over 100clinics, senta 3 za watoto na wanawake, mshirika ya elimu na idara za tafiti 15. Hospitali inahudumia zaidi ya watu milioni 37 kutoka zaidi ya 120 duniani.
Hospitali hiyo inaendelea kuimarisha utumiaji wa teknolojia mpya ambapo hivi sasa, inatumia teknolojia ya upasuaji wa kutumia roboti. Apollo pia ni waanzilishi wa kampeni ya Tender Loving Care (TLC) ambayo inaendelea kuhamasisha matumaini na hali ya urahisi kwa wagonjwa.