Hizi ndizo Sababu za Kujiuzuru Katibu Mkuu Wa Yanga

TIBO yanga

KATIBU Mkuu wa Yanga SC, Dk. Jonas Tiboroha amejiuzulu na tayari amewasilisha barua kwa Mwenyekiti, Yussuf Mehboob Manji. Tiboroha asema kwamba amechukua uamuzi huo ilia pate muda zaidi wa kufanya shughuli zake za Uhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

“Mimi ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha Elimu ya Viungo (PE), na kwa kuondoka Yanga SC maana yake napata wasaa mzuri wa kumtumikia mwajiri wangu, UDSM,”amesema.

Pamoja na Tiboroha kutozama ndani sana juu ya kujiuzulu kwake, lakini inaelezwa alikuwa hana maelewano na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu, Isaac Chanji ambaye kwa sasa ndiye mtu anayesikilizwa na kuaminiwa zaidi na Manji.

TIBOROHA

Kwa upande wake, Tiboroha alipoulizwa kuhusu mahusiano yake na Chanji alisema; “Nilichoandika katika barua yangu ya kujiuzulu ndiyo sababu za msingi, kikubwa ninawapisha watu ambao wanaweza kuiongoza vizuri Yanga SC kuliko mimi,”amesema.

Tiboroha aliingia Yanga SC Desemba mwaka 2014 akichukua nafasi ya Benno Njovu aliyeondolewa kwa tuhuma mbalimbali. Aliingia Yanga SC akitokea Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kama Ofisa Maendelezo ya Ufundi.

Wengi walikuwa wanaripoti kuwa katibu mkuu huyo katangaza kujiuzulu kwa shinikizo na sio maamuzi yake, kitendo ambacho kilifanya mchana wa jana January 23 wapenzi na wanachama wa klabu hiyo wakusanyike makao makuu na kupinga uamuzi huyo katikavyombo vya habari.