KUMI NA TANO SI HABA (PONGEZI)
Pongezi nina zituma, kwako Tedi nawe Nesto
Mu imara kama chuma, kwa upendo wake Kristo
Mungu awape uzima, mkalea na watoto,
Kumi na tano si haba, Mroki nawapongeza.
Mroki nawapongeza, kumi na tano si haba,
Nesto leo umeweza, nyumbani waitwa baba,
Tedi ye hakuteleza, tuli yeye hakuyumba,
Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.
Mungu kawabariki, wana weri kawapa,
Japo home hamshikiki, ulizi wana huwapa,
Ibada mnashiriki, pongezi mi ninawapa,
Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.
Kubwa shukrani kwa mola, mja wetu wa karima,
Alo ziepusha hila, kwetu sisi maamuma,
Tedi waivaa shela, hakupenda dada wema,
Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.
Jala wetu wa Jalalu, wape zaidi hekima,
Mmoja asiwe lulu, mwingini akawa Kima,
Hapo hawatafaulu, kuheshimiana daima,
Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.
Wote mkajidhatiti, kwenye wenu upendo,
Mkipiga Serengeti, msipigane mabindo,
Kuweni watu wa geti, upole uwe mtindo,
Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.
Hizi saba zinatosha, kiu kimenikamata,
Sio vyema kuwachosha, maneno mmeyapata,
Nami nitajibidisha, yenu siri kuipata,
Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.
Mroki Mroki “Father Kidevu
+255 717 002303
mrokim@gmail.com
www.mrokim.blogspot.com