JESHI la Uganda limesema helikopta zake nne zilizokuwa zime ripotiwa kutoweka zikiwa njiani kuelekea Somalia sasa zimepatikana na marubani wake wote wakiwa hai.
Akizungumza msemaji wa jeshi hilo Kanali Felix Kulaigye hakuweza kusema ndege hizo ziko wapi kwa sasa.
Naye msemaji wa jeshi la Kenya, Bogita Ongeri ameiambia BBC kwamba operesheni ya kutafuta ndege hizo ilikuwa imevurugwa na hali mbaya ya hewa na kuongeza kuwa helikopta hizo nne zilikuwa kwenye safari hiyo kutoka nchini Uganda.
Moja ya helikopta hizo ilitua katika mji wa Garissa. Rubani aliyekuwa kwenye helikopta ya pili alizungumza na mamlaka za kenya akisema yuko katika eneo la mlima Kenya lakini hakukukuwa na mawasiliano na helikopta nyingine mbili.
Helikopta hizo za Uganda hutumiwa kusindikiza misafara kutoka angani, katika opereresheni za utafutaji na uokoaji pamoja na kushambulia wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabaab nchini Somalia.
Helikpta hizo ni miongoni mwa ndege ambazo zilikuwa zikielekea Somalia kukipa nguvu kikosi cha Umoja wa Afrika.
Awali msemaji wa jeshi la Uganda Kanali Felix Kulayigye alikuwa amesema kuwa walikuwa wakizitafuta ndege zao mbili aina ya Mi-24 . Alisema ndege hizo ni zile za kufanya mashambulizi.
-BBC