
HELIKOPTA iliyokuwa na abiria 3 na rubani imeanguka eneo la Moshi Bar jirani na Sukuma Land Bar Ukonga na kuua watu wote ndani ya ndege hiyo.

Ajali hiyo pichani. Taarifa za awali zinasema Helikopta hiyo ilikuwa ya kiraia na imeanguka ikiwa safarini.
HELIKOPTA iliyokuwa na watu wanne imeanguka eneo la Moshi Bar jirani na Sukuma Land Bar Ukonga na kuua abiria wote. Taarifa za awali zinasema Helikopta hiyo ilikuwa ya Wizara ya Maliasili na Utalii imegharimu maisha ya marubani 3 wote wa Jeshi la Polisi Tanzania. SP Kidai Kaluse, Insp. Simba Must Simba, PC. Josso Selestine, na Capt. Khalfan. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana mpaka sasa.