Mpiga picha Nancy Borovik aliwapiga picha wazazi wake wakiwa wanapigana na ugonjwa wa kansa. Nancy alivyojua kuwa wazazi wake wote wana kansa, hakujua ni namna gani watachukulia ugonjwa huo, lakini waliweza kusaidiana na kupeana moyo mpaka mwisho.

Walikuwa pamoja katika habari njema na habari mbaya

Hamna kati yao aliyejua mwenzake ana kansa “4th stage”

Howie alijulikana kuwa ana kansa ya “pancreas”

Laurel alikuwa na kansa ya maziwa

Binti huyo, aliwapiga wazazi wake picha wakati wananyoa nywele

Wakiwa njiani kwenda kwenye chemotherapy.

Laurel na Howe walisaidiana sana katika wakati mgumu katika maisha yao

Walifanya kila wawezalo kufurahishana

Pamoja na majaribio yote, Nancy aliweza kushuhudia wakati muhimu sana katika maisha ya wazazii wake

Pamoja na kuwa wagonjwa sana, waliweza kusheherekea harusi ya binti yao

Fungua nikifa, kabla sijazikwa

Baada ya kupambana na ugonjwa wa kansa, Howe alifariki na kumuacha mkewe na binti 3