Hatua za Lala Salama Uchaguzi wa Kenya

Mgombea Uhuru Kenyatta wa muungano wa Jubilee

KINYANG’ANYIRO cha Uchaguzi Mkuu wa Kenya utakaofanyika Jumatatu kimeingia hatua ya lala salama hivi sasa, huku wagombea wakiendelea kuzunguka kwenye majimbo kuomba kura. Kura za maoni zinaonesha ushindani mkali upo kati ya mgombea Uhuru Kenyatta wa Jubilee na Raila Odinga wa CORD.

Mshindani anayewafuata ni Musalia Mudavadi wa muungano wa Amani na anashikilia nafasi ya tatu nyuma ya wawili hao kulingana na kura za maoni. Kwa mgombea kushinda uchaguzi lazima apate zaidi ya asilimia hamsini na takriban asilimia 25 ya kura katika nusu ya majimbo 47.

Miungano ambayo inaongoza kwenye kura zamani inatumia mbinu mbalimbali kuwashawishi wapiga kura kujitokeza siku ya kupiga kura. Muungano wa Cord wake, Raila Odinga, ulisema kuwa unawataka watu 330,000 kuwaombea kura kwa wapiga kura kote nchini.

Bwana Kenyatta amekuwa akiwashawishi wapiga kura kupiga kura mapema kabla ya kuelekea kazini na makwao wakati mgombea mwenza wake William Ruto,amewataka vijana kuhakikisha kuwa marafiki zao na jamaa zao wameweza kupiga kura.

Jimbo la Rift Valley, moja ya majimbo makubwa, ina kauti 14 ikiwa na wapiga kura milioni 3,373,853. Eneo hilo linatazamiwa kama ngome ya William Ruto. Utafiti wa mwisho uliofanywa kuhusu maoni ya watu kuwahusu wagombea wakuu, ulionyesha kuwa Kenyatta angemshinda Raila asilimia 60 kwa asilimia 23. Pande hizo mbili hata hivyo zina matumaini ya kuibuka mshindi.

Kwa upande wake, Muungano wa Jubilee wake Kenyatta umeelezea matumaini makubwa, ukitaka kushinda kiwango kikubwa cha kura. Mkoa wa kati ndio wa pili wenye idadi kubwa zaidi ya wapiga kura na eneo hilo ni ngome ya Uhuru Kenyatta. Kura zote za maoni, zinawaweka zinaonyesha kuwa Kenyatta anaweza kushinda asilimia tisini ya kura katika eneo hilo.

-BBC