Na Salum Mwinyimkuu, Morogoro ZAIDI ya hatimiliki 300,000 za Ardhi zinatarajiwa kutolewa kwenye Wilaya za KILOMBERO, MALINYI na ULANGA mkoani Morogoro kupitia mradi wa kuwezesha Urasimishaji Ardhi wa LTSP, ili kupunguza Migogoro ya Mipaka kwenye Vijiji.
Miongoni mwa Changamoto inayofifiza Juhudi za Serikali kumaliza tatizo la Migogoro ya Ardhi katika Wilaya za KILOMBERO, MALINYI na ULANGA ni Rushwa kwa Baadhi ya Watendaji wasio waaminifu.
Wilaya ya KILOMBERO yenye vijiji 99 imejizolea Umaarufu kwa kuwa na maeneo mengi yenye Utata wa Ardhi,ikihusisha migogoro ya Mipaka baina ya kijiji na kijiji, hifadhi na kijiji pamoja na wakulima na wafugaji.
|