Hatimaye Laurent Gbagbo akamatwa

Laurent Gbagbo akiwa chini ya ulinzi wa majeshi wa UN

Laurent Gbagbo akiwa chini ya ulinzi wa majeshi ya Umoja wa Mataifa baada ya kukamatwa kwenye hoteli moja ambamo alikuwa amejificha mjini Abidjan.

Taarifa zaidi zinasema vikosi vya wanajeshi vinavyo mtii Alassane Ouatarra vimemkamata kiongozi huyo na sasa yupo chini ya ulinzi na amekabiziwa kwa majeshi ya Ouatarra.