Hatimaye Bunge Lazibadili Sheria za Madini Tanzania

Baadhi ya madini yanayopatikana Tanzania

 

BUNGE la Tanzania hatimaye limepitisha sheria mpya mbili na muhimu za uchimbani madini ambapo kwa pamoja zina lengo la kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya madini. Sheria hizo mbili zinafuatia mzozo wa miezi miwili kati ya serikali na Kampuni ya uchimbaji madini ya Uingeraza ya Acacia, kufuatia madai kwuwa kampuni hiyo imekuwa ikikosa kulipa kodi.

Kupitia sheria hizo sasa serikali ina matumaini kuwa wananchi watanufaika kutokana na mali asili ya nchi hiyo. Moja ya sheria hizo inasema kuwa watu nchini Tanzania watakuwa na uhuru wa kudumu kwa mali yao ya asili na serikali kwa niaba ya watu itasimamia mali hiyo. Hadi sasa sheria haikuweza kueleza wasi ni nani ana uhuru wa kusimamia mali asili ya nchi ya Tanzania.

Sheria nyingine inaipa bunge mamlaka ya kutathmini makubaliano yanayofanywa na serikali kuhusu mali asili. Serikali inalaumu kampuni ya Acacia kwa kutofichua kiwango cha madini inachopeleka nje ya nchi na kukosa kulipa kodi ya mamilioni ya dola kwa muda wa miaka 20 imekuwa ikihudumu nchini humo.
Kampuni hiyo hata hivyo imepinga takwimu hizo za serikali ikisema kuwa ikiwa zilikuwa za ukweli, basi Tanzania ingekuwa mzalishaji mkubwa zaidi wa dhahabu na shaba duniani.