Harakati za Uchukuaji na Urejeshaji Fomu kwa Makada wa CCM Leo

Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza na wananchi mjini Chalinze wakati alipotangaza nia yake ya kutetea tena ubunge wa jimbo hilo.

Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza na wananchi mjini Chalinze wakati alipotangaza nia yake ya kutetea tena ubunge wa jimbo hilo.

????????????????????????????????????

Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akisalimiana na Diwania wa Kata ya Bwilingu Bw, Ahmed Masser wakati alipowasili katika eneo la mkutano uliofanyika mji mdogo wa Chalinze jana ukiwa na lengo la kuelezea utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM uliofanywa na Mbunge huyo kwa kipindi cha mwaka mmoja katika huduma za Afya, Elimu, Maji, Miundombinu, Uchumi, Michezo na amaendeleo mengine ya kijamii.

Ridhiwania Kikwete ametanganza rasmi jana katika mkutano huo nia yake ya kutetea jimbo la Chalinze ambapo leo mchana anatarajiwa kuchukua fomu katika ofisi za CCM wilaya ya Bagamoyo tayari kwa kuanza mchakato wa kuwania tena ubunge wa jimbo la Chalinze ili kuendeleza yale aliyokwishayaanza kutekeleza katika kipidi cha mwaka mmoja alipokuwa madarakani.

????????????????????????????????????

Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akisalimiana na wananchi mbalimbali wakati alipowasili katika eneo la mkutano mjini Chalinze.

????????????????????????????????????

Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza jambo na Katibu wake Bw. Idd Swala huku Diwani wa Kata ya Bwilingu Ahmed Nasser akisikiliza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Bw.ndugu Majid Mwanga.

????????????????????????????????????

 Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ndugu Majid Mwanga.

????????????????????????????????????

Diwani wa Kata ya Bwilingu Ahmed Nasser akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jana.

????????????????????????????????????

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ndugu Majid Mwanga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jana.

????????????????????????????????????

Wananchi wa Chalinze wakimsikiliza Ridhiwania Kikwete mbunge wa jimbo hilo hayupo pichani wakati alipokuwa akitangaza nia yake ya kutetea tena kiti cha ubunge wa jimbo la Chalinze.

********************************************************************************************************************

Bi. Chikulupi Njelu Kasaka 
Mgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Mbeya Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto) akikabidhiwa Fomu ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana Mbeya na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu
 Kushoto ni Bw. Moses Mwakibinga Katibu wa Hamasa na Chipukizi Wilaya ya Chunya, Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto)  na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu Baada ya kukabidhiwa Fomu

                                                MFAHAMU BI. CHIKULUPI NJELU KASAKA

*Ni Mwanasheria (wakili) kitaaluma.
*Ni mfanyakazi wa Bunge la JMT.
*Sasa anawania Ubunge wa Viti-maalum (vijana).
*WASIFU WA MGOMBEA: BI. CHIKULUPI KASAKA
ELIMU:
Chikulupi Kasaka ni mzaliwa wa Chunya na babu na Bibi ni wakazi wa Kijiji cha
Mtanila katika Wilaya ya Chunya. 
 Chikulupi alizaliwa mwaka 1986 na kuanza elimu
ya msingi mwaka 1994 katika shule ya Chunya Kati. Chikulupi alimaliza elimu ya
msingi Mkoani Tabora na kuchaguliwa kwenda shule ya Serikali ya Sekondari ya
Wasichana Msalato iliyopo Dodoma ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha nne
mwaka 2000-2004. Mwaka 2005-2007 alijiunga na Shule ya Serikali ya Sekondari ya
Wasichana Loleza iliyopo Mkoani Mbeya. Alishaguliwa kijunga na Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam mwaka 2007 kusomea Shahada ya Kwanza ya Sheria na kumaliza mwaka
2011. Mwaka 2013 alijiendeleza kwa kujiunga na mafunzo ya uanasheria kwa vitendo
na kumaliza mwaka 2014 katika chuo kiitwacho Law School of Tanzania ambapo
baadaye niliapishwa kuwa wakili.
UZOEFU KATIKA UONGOZI:
Chikulupi aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi akiwa anasoma Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam. Alikuwa Mbunge katika Serikali ya wanafunzi – DARUSO.
 Chikulupi alichaguliwa mwaka 2009 kuwa Makamu wa Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa
Afrika Mashariki uitwao East Africa Community Students Union -EACSU.
 Pia likuwa Afisa Mahusiano ya Umma katika Taasisi ya wanafunzi wa Sheria iitwayo
University of Dar es Salaam Human Rights Association –UDHRA. Mwaka 2010
alishiriki mafunzo ya Uongozi kwa Vijana yaliyofadhiliwa na Shirika la
Kijeruman liitwalo Friedrich Ebert Stiftung –FES.
 Pia mwaka 2014 alishiriki
mafunzo ya Viongozi Vijana toka barani Afrika nchini Marekani ambao alisomea
masomo ya Public Management katika chuo cha Howard kilichopo Washington. Pia
nilipata fursa ya kukutana na Rais Barack Obama ambae ni mwanzilishi wa mafunzo
haya.
UZOEFU NDANI YA CHAMA/UVCCM:
Chikulupi Kasaka alijiunga na CCM hasa katika jumuiya ya UVCCM mara tu baada ya
kumaliza elimu ya sekondari 2006. 
Alipokuwa anasomea Shahada ya Sheria Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam alijikita katika shughuli mbalimbali za kuimarisha
chama na mwaka 2010 alichaguliwa Mwenyekiti wa UVCCM tawi ya Abiyan-Chuo Kikuu.
Na mjumbe wa Shirikisho la Vyuo Vikuu wanaCCM, Mkoa wa Dar es Salaam.
KAZI:
Mara baada ya kumaliza chuo kikuu Julai 2011 Chikulupi alifanya kazi katika
Shirika la Wakimbizi katika Mradi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uitwao
International Migration Management Program (IMMP). 
Mwaka 2012 aliajiriwa na
Serikali kama Hakimu Mkazi daraja 2, katika Mahakama ya Mwanzo
Makongorosi-Chunya, Mbeya. Mwishoni mwa mwaka 2012 nilijiunga na utumishi wa
Chama Makao Makuu ya CCM Dodoma. 
Nilipangiwa kufanya kazi za Chama katika
Upande wa Bunge hasa za kisheria. Tangu kipindi hicho mpaka sasa Chikulupi
anafanya kazi kama Msaidizi wa Katibu wa Wabunge wote wa CCM, Bungeni Dodoma.
VIPAUMBELE:
Chikulupi Kasaka anaomba ridhaa yako ili aweze kuwawakilisha vijana wa Mkoa wa
Mbeya katika nafasi ya Uongozi wa Kitaifa kupitia ngazi ya Ubunge wa Viti
Maalum-Vijana. 
Kama mkazi wa Mbeya naamini vijana wa Mbeya wanauwezo, nguvu,
bidii na jitihada katika shughuli zao za kila siku. Lakini mimi nitapigania kuwapatia
vijana wa Mbeya fursa nyingi zaidi katika vipaumbele vifuatavyo: 
ELIMU, AJIRA, MICHEZO, UTALII na AFYA.
ANAOMBA UMUUNGE MKONO KWA FURSA ZAIDI KWA VIJANA WA MKOA WETU WA MBEYA.

****************************************************************************************************************

Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Anastaz Mpanju ambaye pia alikuwa Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba Mpya amejitokeza hii leo sambamba na wana CCM wengine katika safari ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Kawe Wilaya ya Kinondoni.
Akizungumza na Father Kidevu Blog, katika ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Mpanju amesema huu ni wakati muafa kwake kuwatumiakia wana Kawe. Mpanju ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, amesema wanakawe wananafasi sasa ya kuandika historia  ya aina yake si tu kumchagua mtu mlemavu bali kumchagua, kijana na mchapakazi mwenye uwezo wa kutetea na kuwasilisha hoja za kuleta maslahi kwa kawe na taifa.
“Huu ni wakati wa wananchi wa Kawe kuandika historia ya aina yake, sit u kwa kumchagua mtu mwenye ulemavu kuwaongoza bali kijana mwenye uwezo wa kutetea hoja na maslahi yua wananchi na taifa kwa ujumla,”alisema Mpanju.
Mpanju amekuwa ni mwananchi wa 16 kujitokeza kugombea jimbo la Kawe na ni mwana CCM wa
39 kujitokeza kuomba ridhaa ya chama kuteuliwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho.
Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Mpanju akizungumza na wanahabari . Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe akimsaidia kutia saini ya dole gumba Mpanji.
Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Mpanju akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe, kwaajili ya  kuomba ridhaa ya wana CCM Kinondoni kumteua kugombea Ubunge Jimbo la Uchaguzi la Kawe katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athumani Sheshe (pichani), amempongeza Mpanju kwa uamuzi wake huo na kusema kuwa anatekeleza moja ya kanuzi na sheria za Chama kuwa watu wote ni sawa na walemavu wanahaki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa vipongozi.

“Mimi nitoe wito kwa watu wote wenye ulemavu nchini ambao wanasifa na vigezo vinavyotakikana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini wajitokeze na kufanya hivyo na watatendewa sawa sawa na wengine bila ubaguzi au unyanyapaa,”alisema Sheshe.

**********************************************************************************************************************

Mwansheria na Kada wa Chama cha Mapinduzi, Emmanuel Makene (katikati) akiwa ameambata na mkewe Dk. Sarah Makene kurejesha fomu za kuomba ridhaa ya wana CCM Kinondoni kuteuliwa kugombea Ubunge katika Jimbo la Kinondoni. Anaepokea fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe. Wengine ni wapambe wa mgombea huyo waliomsindikiza kurejesha fomu hizo leo.
Emmanuel Tamila Makene ambae ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya na Katibu wa Usalama na Maadili taifa wa Umoja wa vijana (UVCCM) akisaini kitabu cha kurejesha fomu huku mkewe Dk Sarah Makene akimwangalia kwa makini na Katibu wa CCM Wilaya akikagua fimu. Dk Sarah Makene ni Daktari katika Hospitali ya Mwananyamala anaeshughulika na wagonjwa wa Ukimwi na wWaathirika na dawa za kulevya.
Dk Sarah Makene ni Daktari katika Hospitali ya Mwananyamala anaeshughulika na wagonjwa wa Ukimwi na wWaathirika na dawa za kulevya, akipeana mkono na Katibu wa CCM Wilaya baada ya kupokea fomu za Muwewe.

Makene akiwa na Mkewe Dk Sarah pamoja na rafiki yao baada ya kurudisha fomu.

Makene akiwa na Mkewe Dk Sarah na marafiki zao baada ya kurejesha fomu.
*****************************************************************************************************************
Mtoto wa Komando Dk Salmin Amour Juma Amini Salimini achukua Fomu kogombea Jimbo la Mkwajuni Zanzibar akiwasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kaskazini A Gamba kwa ajili ya kuchukua Fomu kogombea Jimbo hilo, akisalimiana na Wananchi waliopo hapo.
Mama wa Amini Salimi Bi Khadija Kasimi akisalimiana na Katibu Msaidi wa Ofisi ya CCM Wilaya Kaskazini A Unguja alipofika katika Ofisi hizo kumshindikiza Mtoto wake kuchukua Fomu ya Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Zanzibar.

Katibu Msaidizi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Kaskazini Unguja Ndg Shafi Hamad akitowa maelezo kwa Mgombea kabla ya kumkabidhi fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Jimbo la Mkwajuni

Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Amini Salimini akihesabu fedha kwa ajili ya kulipia Fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge kupitia CCM katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kaskazini Unguja Gamba.
Katibu Msaidi Ofisi ya CCM Wilaya ya Kaskazini a Unguja Ndg Shafi Hamad akimkabidhi Fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Mkwajuni Amini Salimini, baada ya kukamilisha taratibu zote za malipo na kutimiza masharti ya Chama cha Mapinduzi.
Katibu Msaidi wa CCM Wilaya ya Kaskazini A Unguja akitowa maelezo kwa mgombea baada ya kumkabidhi fomu hiyo Ndg Amini Salimini.
Mgombea wa Jimbo la Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Unguja  Amini Salimini akiwa katika picha ya kumbukumbu na familia yake baada ya kuchukua Fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni kwa tiketi ya CCM, akiwa katika Ofisi za CCM Gamba.
Amini Salimini akiwa katika picha ya pamoja na familia yake baada ya kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mkwajuni Zanzibar.Akionesha fomu yake baada ya kukabidhiwa kwa hutua za ujazaji
Amini Salimini akitoka katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kaskazini A Unguja baada ya kuchukua fomu hiyo akionesha kwa wananchi walioko katika eneo hilo.
Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Unguja Amini Salimini akiwa na Mtoto wake wa Kwanza wakishikilia fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuiwakilisha CCM katika Jimbo la Mkwajuni Zanzibar.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Amani Salimini akiomba dua katika makaburi ya Wazee wake huko Kidombo baada ya kuchukua Fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Zanzibar

Amini Salimini akipata dua kutoka kwa Wazee wa Kijiji cha Kidombo Mkwajuni baada ya kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge wa Jimbu la Mkwajuni Zanzibar kupitia CCM.
*********************************************************************************************************************
Mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mwinchum Msomi  akisalimiana na mgombea Ubunge kupiti chama hicho Dk. Faustine Ndugulile anaye tetea Jimbo lake walipokutana Ofisi za chama hicho Wilayani  Temeke Dar es Salaam jana.
Mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mwinchum Msomi, akimkabidhi Pesa  Katibu Umoja wa Vijana Wilaya ya Temeke Yona Sengerema , kwaajili ya malipo ya uchukuaji wa  fomu.
 Mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mwinchum Msomi, akisaini fomu mbalimbali mbele ya   Katibu Umoja wa Vijana Wilaya ya Temeke Yona Sengerema.
Katibu wa Umoja wa Vijana wilaya ya temeke akimkabidhi Fomu  Mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mwinchum Msomi alipofika ofisini hapo Dar es Salaam jana kuchukua fomu hizo.